MKOA WA KASKAZINI UNGUJA
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba Zanzibar inahitaji kuwepo mfumo na utaratibu
bora wa matumizi na usimamizi sahihi wa
ardhi ili kuwawezesha wananchihi kufaidika vyema na rasilimali hiyo ili waweze kupambana
vyema na umasikini.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko Mkwajuni wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja alipohutubia wananchi na wafuasi wa chama hicho katika mkutano
wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa mikutano mbali mbali ya ACT - Wazalendo
inayoendelea katika mikoa mbali mbali Unguja na Pemba.
Aidha amefahamisha
kwamba iwapo serikali itakuwa na mfumo bora na sahihi utasaidia wananchi wanaomiliki rasilimali hiyo kupata kipato
kikubwa zaidi kutokana na ukodishaji, huku serikali nayo ikaweza kufaidika
katika kusanyaji wa kodi inayotokana na aradhi
hiyo.
Mhe. Othman
ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar, amefahamisha kwamba ardhi ni rasilimali muhimu ya umma ambayo mwananchi
anayemiliki anahitaji kuwezeshwa kwa kuandaliwa
utaratibu bora utakaleta tija na faida kubwa kupitia uwekezaji wa aina mbali mbali unaofanywa
na wawekezaji wa ndani nba nje ya nchi.
Aidha amefahamisha
kwamba utaratibu uliopo sasa hauna tija na manufaa makubwa kwa wananchi ambao
ardhi zao zinatumika kwa uwekezaji jambo ambalo linachangia kutofanikiwa katika
kupambana na umasikini.
Mhe. Othman
amesema kwamba sera bora na mipango mizuri ya usimamizi wa rasilimali hiyo ni
njia sahihi ya kumuezesha mwananchi wa kawaida kuweza kupata kipato
kikubwa zaidi na kujikwamua na tatizo la
umasikini kama zinavyofanya nchi mbali mbali duniani.
Mhe. Othman
amesema kwamba hatua hiyo ni muhimu kwani itasaidia sana katika jitihada za ujenzi wa Zanzibar mpya ambayo itawafanya wananchi
kuondokana na tatizo la umasikini sambamba na kudumisha , umoja Amani na
mshikamano wa kweli.
Amesema
kwamba ni muhimu kuzingatiwa kwa suala hilo kwani uchumi , maendeleo bora na amani ya kweli katika nchi
yoyote duniani yanatokana na wananchi kuwa na mamlaka ya kamili ya kuwachagua
na kuwawajibisha viongozi wao katika ngazi mbali mbali.
Akizungunzia
suala la Muungano, Mhe. Othman amesema kwamba ni muhimu kuwepo Mungano wenye
mkataba madhubuti unaotoa na kusimamia
maslahi yenye uwiano sawa kwa pande mbili za muungano ili taija ya suala hilo iweze kupatikana na kuwafaidisha wote.
Mhe. Othman
amewata wananchi na wafuasi wa chama hicho kuendelea kuinunga mkono ACT- ili
kiweza kuwa na uwezo na mamlaka ya
kusimamia ipasavyo maslahi ya Zanzibar na kuchangia maendeleo ya wananchi
katika nyanya mbali mbali.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Ismali Jussa Ladhu, amesema nchi
haiwezi kupiga hatua na kuwa na maendeleo iwapo hakutomkuepo na jitihada za kupinga vitendo vya ufisadi hasa katika taasisi za serikali nchini.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa ya Chama hicho Pavu Juma Abdalla,
amesema kwamba utaratibu usiofaa wa usimamizi wa ardhi unachangia sana
kuwafanya wanawake wa Zanzibar kuwa ndio waathirika wakubwa wa masuala hayo hasa
kwa vile wao ndio wakulima wakubwa wanaosaidia familia kupitia juhudi za kilimo
cha aina mbali mbali.
Mapema Mhe.
Othman alifika huko Donge Muwanda
Kuifariji familia ya Bwana Mohammed aliyefiwa na watoto watatu hivi karibuni
kwa kuzama kwenye mashimo yenye maji, na pia Donge Kipange na kutembelea kuwapa
pole wagonjwa na wafiwa katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja .
Mwisho
Kitengo cha
Habari
Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Julai
16,2023.
No comments:
Post a Comment