Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ahudhuria Gwaride la Jeshi la Wanamaji la Urusi

Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin Putin wakati alipohudhuri  gwaride la Jeshi la Wanamaji la nchi hiyo  lililofanyika St. Petersburg nchini Urusi, Julai 30, 2023. Katikati ni mkewe Mama Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati alipohudhuri  gwaride la Jeshi la Wanamaji la nchi hiyo lililofanyika St. Petersburg nchini Urusi, Julai 30, 2023. Kushoto ni mkewe Mama Mary Majaliwa.
 Rais wa Urusi Vladimir Putin akipokea heshima ya gwaride la jeshi la wanamaji la nchi hiyo lililofanyika katika jiji la St. Petersburg nchini Urusi, Julai 30, 2023. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumapili, Julai 30, 2023) alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Maonesho ya Gwaride Maalum la Jeshi la Wanamaji la Urusi yaliyofanyika Senatskaya Marina, St. Petersburg, Urusi.

 

Viongozi hao ni wale walioshiriki Mkutano wa Pili wa Kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi jijini St. Petersburg, Urusi ambako yeye alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Maonesho hayo yamefanyika ikiwa ni siku ya Jeshi la Wanamaji la Urusi na maadhimisho  ya kukumbuka kuanzishwa kwa jeshi hilo ambayo hufanyika Julai 30, kila mwaka.

 

Katika maonesho hayo Rais wa Urusi, Vladmir Putin alipita kwenye boti maalum akiwasalimia wananchi waliojipanga kwenye kingo za mto Bolshaya Neva na kupokea salamu za kijeshi. Alipomaliza akavushwa na boti ndogo kwenda kwenye jukwaa maluum na kuhutubia Taifa.

 

Baada ya hapo meli na boti za kivita zilipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima. Kisha akaenda kuwasalimia mmoja baada ya mwingine viongozi wa Afrika waliohudhuria maonesho hayo na baadaye alipanda nao kwenye boti hiyo maalum.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, JULAI 30, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.