Na. Omar Hassan -ZANZIBAR 07/08/2023
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema uwajibikaji na utoaji wa haki kwa Wakaguzi wa Shehia kutaleta mabadiliko na kuunda jamii salama, imara na yenye mshikamano.
Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Shehia wa Mikoa mitatu ya Unguja huko katika Kambi ya Polisi Ziwani Wilaya ya Mjini Unguja, ameeleza kuwa uwepo wa Wakaguzi wa Shehia kunatoa matumaini kutatua matatizo ya jamii, kuzuwia na kupunguza uhalifu, kuimarisha uwajibikaji wa Polisi na kupunguza hofu ya uhalifu.
Mratibu wa Mafunzo hayo Mrakibu wa Polisi Dkt.Ezekiel Kyogo kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma amesema mafunzo hayo yatawajenga uwezo Wakaguzi hao wa Shehia kuelewa vizuri Falsafa ya Polisi jamii na kuwa na uwezo wa kuifanyia kazi kwa ufanisi.
Kwa upande wake Veronica Fubile kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP amesema shirika hilo linasaidia kufanya Mafunzo hayo ni kutoa mashirikiano ya kiusalama ili kukuza Maendeleo ya Nchi.
No comments:
Post a Comment