MUONEKANO wa Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja, kilichofunguliwa leo 14-8-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu)
AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Viongozi wengine , alipowasili katika viwanja vya Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo hicho uliofanyika leo 14-8-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja na (kushoto ) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kukifungua Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 14-8-2023, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Iddi Ali Ame na (kushoto kwa Rais) Mbunge wa Jimbo la Bumbwini Zanzibar Mhe. Mbarouk Juma Khatib na Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Mhe. Mtumwa .P.Yussuf na Waziri wa Afya Zanzibar. Mhe.Nassor Ahmed Mazui.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Muunguzi Mkunga katika Kituo cha Afya Makoba.Rehema Ramadhan Abdalla, akitowa maelezo wakati akitembela chumba cha kuzalia katika Kituo hicho, baada ya kukifungua leo 14-8-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya mashine ya Kisasa ya kung'olea meno (Dental Unit) kutoka kwa Daktari wa meno Dkt. Kassim Salum Mohammed, alipotembelea Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja,baada ya kikifungua leo 14-8-2023, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiangalia mashine ya kupimia presha wakati Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Dkt. Fatma Ame Salum akimpima Bi. Fatma Mtumweni Kondo, alipofika katika kituo hicho kwa kupata huduma ya Afya,wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho uliofanyika leo 14-8-2023.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment