Habari za Punde

Ujenzi wa kiwanda Cha Serikali cha Mwani Chamanangwe wafikia asilimia 90Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt Aboud Suleiman Jumbe, tarehe 7 Agosti 2023 amefanya ziara katika eneo la ujenzi wa kiwanda Cha Serikali cha Mwani kilichopo Chamanangwe na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambapo kwa sasa kimefikia asilimia 90% ya ujenzi kwa hatua ya awali.

Akiwa na wasimamizi na wahandisi wa ujenzi wa Kiwanda hicho Dkt Jumbe alisema kuwa Chamanangwe inaelekea kuwa kitovu kikubwa cha viwanda vya usarifu wa mwani pamoja na utengenezaji wa bidhaa za mwani na kusafirisha bidhaa za mwani katika masoko ya Kimataifa.
Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi alitangaza kuja kwa mradi mwengine mpya wa mwani unaofadhiliwa kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Korea (KOICA) na ambao pia, katika mojawapo ya utekelezaji wa program yake, utajenga kiwanda cha ziada cha kutengeneza bidhaa zilizomalizwa (finished products) za mwani. Kiwanda hicho kinatarajiwa pia kujengwa kisiwani Pemba.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.