Habari za Punde

Waratibu Wizara ya elimu watakiwa kubadilika

Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Mwalimu Moh’d Nassor Salim amewataka Waratibu wa Idara na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Wizara ya Elimu Kuongeza bidii katika kuwajibika ili kuendana na kasi ya Mabadiliko katika Maendeleo ya Elimu.

Ameyasema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa kipindi cha TUWAJIBIKE uliowashirikisha Waratibu na Wakuu wa Vitengo iliyofanyika katika Ukumbi wa Afisa Mdhamini Chake Chake Pemba.
Mwalimu Moh’d amesema kila mmoja kwa nafasi yake anawajibu wakujitathmini na kuchukua hatua stahiki za kuongeza kasi ya uwajibikaji ili kuthamini jitihada za Mh. Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi za Kuipa Kipaombele Sekta ya Elimu.
Akizungumzia Kipindi cha TUWAJIBIKE kinachotarajiwa kurusha hewani kila wiki kupitia Radio Elimu FM Afisa Mdhamini amesema nivyema maudhui ya kipindi hicho yawe yakuihamasisha jamii katika kutambua wajibu wao katika uwajibikaji.
Akifafanua Zaidi Mwalimu Moh’d amesema kwamba Wizara ya Elimu inakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo kupitia kipindi hicho jamii itapata fursa ya kuziona na kuzitafutia ufumbizi.
Afisa Mdhamini ameahidi kutoa Mashirikiano ya Dhati katika kuunga mkono utekelezaji wa shughuli mbali mbali za uendeshaji na uandaaji wa vipindi mbali mbali vya Radio Elimu FM.
Kwa upande wake Mratibu wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji Mwalimu Harithi Bakari Waziri akimkaribisha Afisha Mdhamini kuzindua kipindi hicho ametoa pongezi zake za dhati kwa uongozi wa Radio Elimu FM kwa kuandaa vipindi vinavyoendana na mahitaji ya jamii ya sasa.
Aidha Mwalimu Harithi amewashauri waandaaji wa kipindi hicho kukipa mawanda mapana na kujikita Zaidi katika Nyanja mbali mbali zinazoigusa jamii na Taifa kwa ujumla.
Nae Afisa kutoka Kitengo cha Habari katika Elimu Nd. Ali Othman ameishukuru Wizara ya Elim una Mafunzo ya Amali kwa Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Kitengo hicho.
Aidha amewashukuru waratibu na Wakuu wa Vitengo kwa kutoa mapendekezo yao juu ya namna bora ya kuandaa kipindi cha TUWAJIBIKE.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.