Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Nd. Khamis Abdullah Said amesema Wizara ya Elimu Kupitia Chuo Kikuu Cha Taifa SUZA inampango wa kuanzisha Kitivo Cha Taaluma ya Ubaharia.
Nd. Khamis aliyasema hayo alipokutana na Mkufunzi wa Chuo Cha Ubaharia Cha Dar es Salam Kepteni Desm Damford wakati wa Maonesho ya Elimu ya Juu Kisiwani Pemba yaliyofanyika katika Kiwanja Cha Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema kwakua DMI nichuo pekee Cha Ubaharia hapa Tanzania Kitivo kitakachoanzishwa katika Chuo Kikuu Cha Taifa SUZA kitaweza kupata Wataalamu Wakukiendesha kutoka Chuoni hapo.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Chuo Cha Ubaharia kutoka Dar es Salam Kepten Desm Damford ameishauri jamii ya Kizanzibari kujifunza taaluma ya usalama wa bahari kutokana na shughuli kuu za Wananchi wa Visiwa Vya Zanzibar kujikita kwenye eneo la bahari.
Amesema Kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelekea nguvu zake katika dhana ya Uchumi wa Buluu ambao lengo la kuwakomboa wananchi ikiwemo wakulima wa zao la mwani hivyo kuna haja kubwa ya kupata mafunzo ya usalama kwenye kazi zao.
Mkufunzi huyo akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Chuo cha DMI ameahidi kutoa mashirikiano ya dhati kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanikisha kuanzishwa kitivo cha Taaluma ya Ubaharia katika Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.
Awali Afisa Usajili Rehema Athumani Juma amesema DMI ni Chuo pekee Nchini Tanzania kinachotoa taaluma ya Usalama wa Bahati na kwenda sambamba ya Sera ya Uchumi wa Buluu.
Amewataka Wanafunzi Wanaopenda kujiunga na Chuo hicho kuchangamkia fursa na kuwahakikishia kwamba DMI nichuo kinachodahili Wanafunzi Wenye sifa za kawaida Kama Vyuo nyengine Nchini.
Nao baadhi ya walimu na wanafunzi wamesema kupitia maonesho hayo wamepata furusa za kupata uwelewa na kutambua fani mbali mbali ambazo zitawawezesha kujiendeleza kiuchumi kwa kujiajiri au kuajiriwa hususan kupitia eneo la bahari.
No comments:
Post a Comment