Watendaji wa Mradi wa wa kupinga vitendo vya udhalilishaji (GBV) wakimsikiliza mwathirika wa Vitendo vya udhalilishaji wakati akitoa maelezo juu ya msaada aliyopatiwa na wanaharakati wa mradi huo unaosimamiwa na TAMWA Zanzibar huko Jumbi Wilaya ya Magharibi B,Mkoa wa Mjini Magharibi.
PICHA NA FAUZIA MUUSA
NA FAUZIA MUSSA MAELEZO
Waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wameiomba TAMWA Zanzibar kuishajiisha Serikali kutoa adhabu kali kwa watoto wanaokinza na Sheria ili kukomesha Vitendo hivyo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa kupinga vitendo vya udhalilishaji GBV wamesema kupitia TAMWA mambo mengi juu ya kupambana na vitendo hivyo yamefanyika ikiwemo kubadilishwa kwa sheria za kupambana na matukio ya udhalilishaji na kuanzishwa kwa mahakama maalum ya vitendo vya udhalilishaji hivyo endapo watalisimimia vyema suala la watoto wanaokinzana na sheria linaweza kuangaliwa upya.
Walisema asilimia kubwa ya watoto hao hupatiwa adhabu ndogo ikiwemo kifungo cha Miezi 3 na faini ya shilingi laki mbili na nusu ,jambo ambalo haliwaadabishi watoto hao na kuwapa uthubutu wakurejea tena Vitendo hivyo siku hadi sku.
"Mtoto kadhalilishwa na kuharibika vibaya Mzee anatumia gharama kubwa kumtibu na kufatilia kesi Zaid ya miaka 2 siku ya hukumu mtoto anahukumiwa miezi 3 na faini laki mbili na nusu,ambayo laki moja na nusu ni ya Serikali laki moja ndio ya muathirika haikidhi kabisa gharama za kufatilia kesi na matibabu ,wala haifuti machungu ya waathirika wa matukio hayo."Walisema Waathirika hao.
Walisema mara nyingi Vyombo vya Sheria huwahurumia watoto waliofanya vitendo vya udhalilishaji na kusahau athari nyingi wanazopata watoto wanaotendewa vitendo hivyo.
“Mtoto aliefanya vitendo vya udhalilishaji analipiwa faini na wazazi wake hivi tunamuadhibu mototo au mzazi bila ya kupewa adhabu kali yeye kama yeye ataendelea tena na tena kufanya vitendo hivyo”Walishauri Waathirika hao
Hata hivyo waliomba Serikali kuweka chuo maalum cha Mafunzo kwaajili ya watoto wanaokizana na Sheria (Nunda) pamoja na vituo vya kurekebisha Tabia ili kudhibiti watoto hao kuendelea kufanya vitendo hivyo.
Mbali na hayo walioomba TAMWA Zanzibar kuendelea kutoa Elimu ya Saikilojia kwa waathirika wa vitendo vya udhalilishaji ili kuwasaidia kuondakana na athari mbali mbali zinazojitokeza ikiwemo kuathirika kisaikolojia Jambo linalosababisha kushindwa kufanya harakati zao za kimaendelo.
Vile vile Waliishauri jamii kuacha kuwanyanyapaa watoto walioathiriwa na vitendo vya udhalilishaji kwani kunapelekea kushindwa kushiriki katika mambo muhimu ya kijamii ikiwemo kupata haki ya elimu.
Awali waliwashukuru wanamtandao wa kupinga vitendo vya udhalilishaji kwa kuwajengea uthubutu wa kutoa taarifa na kusimamia kesi zao, na kuiomba TAMWA Zanzibar kuleta miradi mengine itakayoendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji hadi kufikia malengo ya kumaliza vitendo hivyo Nchini.
Akizungumza katika ziara hiyo Ofisa Mkuu wa Mawasiliano kutoka TAMWA Zanzibar Sophia Ngalapi alisema katika ziara hiyo wameona mafanikio mbalimbali ya mradi ikiwemo wananchi kufurahia utekelezaji wa TAMWA na uwepo wa wanamtandao sambamba na kuthami mchango unaotolewa na watu hao katika kupambana na vitendo vya udhalilisha.
Alieleza kuwa zaiara imeonesha jamii hairidhishwi na hukumu zinazotolewa kwa washitakiwa waliochini ya miaka 18 kwani haiendani na machungu ya Waathirika ,hivyo TAMWA Zanzibar itakaa na wadau wa kupinga vitendo vya Udhalilishaji kushauriana katika kuliangalia upya suala hilo ili jamii iweze kupata haki zao.
Katika ziara hiyo watendaji wa mradi wa GBV waliwatembelea waathirika wa Vitendo vya Udhalilishaji katika maeneo mbali mbali ya Mikoa ya Unguja ikiwemo Jendele,Mitakawani,Mahonda,
No comments:
Post a Comment