Habari za Punde

Kikao cha Waheshimiwa Mawairi Kujadili na Kukabiliana na Maafa Endapo Yatatokea

Naibu Waziri Mkuu na Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Ukonga Mhe. Jerry Silaa Mwongozo wa kubabiliana na madhara ya El nino leo katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika JIjini Dodoma Leo Tarehe 13 Oktoba.

NA, MWANDISHI WETU – JIJINI DODOMA

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko ameelekeza kila sekta kuchukua hatua kwa kuzingatia majukumu ya sekta husika katika suala zima la utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Dharula wa kukabiliana ma Madhara yatokanayo na EL Nino.

 Ameyasema hayo mapema Leo 13 Oktoba Jijini Dodoma alipokuwa katika kikao cha wahemishimiwa mawaziri  kilichohusu Pamoja wa utekelezaji wa mpango wa Taifa wa wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino.

 

Baadhi ya maelekezo yaliyotolewa ni Pamoja na sekta husika kuainisha na kuandaa rasilimali za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa endapo yatatokea kwa kila sekta kushiriki kikamilifu katika eneo lake, na kutambua maeneo hatarishi yenye viashiria vya kuathirika na maafa na kuandaa mipango ya kuzuia madhara na kukabiliana na maafa endapo yatatokea.

 

Aidha, Mhe. Bitekoe ameelekeza wananchi kuelimishwa na kuhimizwa kuhama kwenye maeneo hatarishi na kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo salama  Pamoja na umuhimu wa kuweka akiba ya chakula na kulima mazao yanayotumia maji mengi, kueleimishwa  juu ya hatua za kuchukua tahadhari ili kuokoa maisha na mali.

 

Pamoja hilo sekta husika zimetakiwa kuandaa na kutekeleza mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea.

 

Kwa upande Wake Waziri wa Nchi Anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, alisema Pamoja na mambo mengine,  Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania iliandaa na kufanya Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Hali ya Hewa uliopokea Taarifa ya Mwelekeo wa Mvua za Vuli (Oktoba – Desemba), 2023 kutoka Mamlaka hiyo, kujadili madhara yanayoweza kutokea na kuainisha hatua za kuchukua, tarehe 22 Agosti, 2023

“kushirikiana na Wizara za Kisekta, Ofisi Waziri Mkuu imeandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Nino kwa kipindi cha Septemba 2023 hadi Juni 2024 kwa kushirikisha sekta husika na wadau.” Alibainisha

 

Awali, akiongea katika Mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa, Dkt. Ladslausi Chang’a alisema kuwa tathmini ya hivi karibu inaonesha kuwa matukio ya El nino yataongezeka kwa idadi na ukubwa wa matukio kadiri ambavyo joto la dunia linavyoendela kuongezeka.

“kama tulivyotoa utabiri mapema kuwa mfumo wa mvua za vuli utachangizwa na mvua za El nino kwa mwaka huu wa 2023. Alisema.”

Aliendelea kusema Mvua ya El nino ya mwaka huu 2023 inaendana kwa mwenendo wake na El nino ya mwaka 1997 na ya mwaka 2006, “Tofauti yake na ile ya 1997 ilikuwa na nguvu sana na iliendana na mfumo wa bahari ya hindi ambao ulikuwa na nguvu sana hivyo, tunaendelea kufuatilia mabadiliko katika  bahari zote.” Alisisitiza. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao cha wahemishimiwa mawaziri  hawapo katika picha, kilichohusu utekelezaji wa mpango wa Taifa  wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino, kilichofanyika Jijini Dodoma. 

Waziri wa Nchi Nayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kikao cha Mawaziri kilichohusu utekelezaji wa mpango wa Taifa  wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino, kilichofanyika Jijini Dodoma 

Picha ya Pamoja Ikimuonesha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko, Mawaziri wa  kisekta pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi baada ya kikao cha Mawaziri kilichohusu utekelezaji wa mpango wa Taifa  wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino, kilichofanyika Jijini Dodoma Leo 13 Oktoba 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.