Habari za Punde

Mbeto atembelea skuli ya sekondari ya Hasnu Makame

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, akizungumza na Viongozi na Wanafunzi(Hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja, ambayo jengo la kulala Wanafunzi wa Kike liliungua kwa ajali ya moto mnamo tarehe 12/10/203,leo tarehe 15/10/2023  amefanya ziara hiyo kwa lengo la kuwatembelea na kuwapa pole wanafunzi hao.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis,akikagua jengo la wanafunzi wa kike lililoungua kwa ajali ya moto katika skuli ya sekondari ya Hasnuu Makame iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja.
 

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.


KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Khamis Mbeto Khamis amesema CCM itaishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuharakisha ukarabati wa  nyumba ya kulala wanafunzi iliyoungua moto hivi karibuni katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame,iliyopo Wilaya ya Kusini Unguja. 

Kauli hiyo ameitoa leo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua Skuli hiyo huko Wilaya ya Kusini Unguja,amesema Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa uongozi wa wilaya hiyo pamoja na wanafunzi kwa ujumla na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu katika wakati huu ambao Chama na Serikali wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kufanya ukarabati na kurejesha huduma mbalimbali skulini hapo.

Mbeto,amewasihi viongozi wa Wilaya hiyo kufanya juhudi binafsi za kuhakikisha wanafunzi wote wanaendelea na masomo hasa wale waliopo katika kambi kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato Pili na Nne ili waendelee kupata huduma za kielimu.

"Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali hii ya kuungua kwa moto nyumba ya kulala wanafunzi wetu wa kike katika Skuli ya Hasnuu Makame, tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi katika kuchukua hatua za haraka Ili wanafunzi waendelee na masomo yao.",alisema Mbeto.

Katika maelezo yake Mbeto,ameahidi kuwa CCM itatoa mchango ili kuunga mkono juhudi za kuhakikisha wanafunzi wa Skuli wanaendelea kupata elimu bora.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Rajab Mkasaba,alisema ajali hiyo ilitokea Octoba 12,mwaka 2023 majira ya usiku wa saa 2:00,na chanzo cha moto huo inasadikika kuwa itilafu ya umeme.

DC.Mkasaba,alisema Serikali inaendelea na juhudi za kufanya tathimini kwa ajili ya kujua gharama halisi za matengenezo hayo ili kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa na wanafunzi wanaendelea na masomo.

Aliwaomba wadau wa maendeleo ,wafanyabiashara maarufu pamoja na watu wenye uwezo kutoa michango ya kusaidia Skuli hiyo ili iweze kumudu gharama mbalimbali za mahitaji ya wanafunzi hao ambao vifaa vyao vyote viliungua kwa moto.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo,Bakar Mohamed Ali,alisema kwa makisio ya awali vifaa vya wanafunzi na Skuli vilivyoungua moto vinagharimu kiasi cha milioni 115.

Nyumba hiyo ya kulala wanafunzi wa kike ilikuwa na vyumba 13 na vyoo 10 ambapo jumla ya wanafunzi 135.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.