Makamu
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na Mjumbe wa Bodi
ya wadhamini wa Chama hicho Mohammed Khamis (Kalipso) wakati Mhe, Makamu
alipowasili katika viwanja vya Daya Mtambwe kwa ajili ya ufungaji wa kampeni
kuelekea uchaguzi Mdogo wa kiti cha uwakilishio wa Jimbo la Mtambwe Kaskazini
Pemba ( Picha na ofisi ya Makamu wa Kwsanza wa Rais wa Zanzibar.)
Makamu
mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman akizungumza huko katika Viwanja vya Daya Mtambwe
kaskazini Unguja katika mkutano wa hadhara wa ufungaji wa Kampeni za uchaguzi
mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe unaotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa
kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( kulia), akinyanyua
mikono kumuombea kura Dk. Mohammed Ali Suleiman ambaye ni wa chama cha ACT katika kinyanganyiro cha
uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Kaskazini Pemba . Mhe. Othman amemdadi mgombea
huyo kwenye viwanja vya Daya Mtambwe katika kutano wa hadhara wa ufungaji wa
Kampeni za uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Oktoba 28, 2023. (
Picha na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar).
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mhe. Othman
Masoud Othman akinywa kahawa aliyokaribishwa na wenyeji wake katika Baraza ya
wazee Huko Daya Mtambwe wakati Mhe. Othman alipotembelea baraza hiyo na kuonana na kuwajulia hali
wazee wa baraza hiyo. Kulia kwa makamu
ni Mwenyekiti wa Baraza Mzee Hamad Omar Mohammed na Mjumbe wa Baraza hiyo Mzee
Mohammed Khatib Juma(makomba) 9 Picha
na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema ni
muhimu kwa watu wa Jimbo la Mtambwe watakaoshiriki uchaguzi mdogo wa Kiti cha
uwakilishi wamchague mgombea wa chama hicho kwa kuwa ndio sauti ya wanzibari
katika kufanikisha mageuzi ya kweli kisiasa na kukuza maendeleo ya kidemokrasia
jambo litakalosaidia kufanikisha vita dhidi ya umasikini.
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo huko Daya Mtambwe aliponadi na kumuombea kura
mgombea wa uwakilishi wa chama hicho Dk.Mohammed Ali Suleiman katika
uchaguzi mdogo Jiombo hilo utakaofanyika
Jumamosi ya tarehe 28 mwezi huu kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo
hilo marehemu Habib Mohammed mnamo mwezi Machi mwaka huu.
Amesema
kwamba Baraza la wawakilishi ni chombo muhimu kinachotetea haki za wananchi na kwamba
mgombea huyo ni chaguo sasa hasa kwa vile ubadhirifu mkubwa umekuwa
ukifanywa katika eneo la manunuzi na kwamba
iwapo watamchagua na mbali na kuwa sauti ya wazanzibari waliowengi lakini pia
ataweza kulisimamia kwa kulisemea vyema eneo hilo kwa vile ni mbobevu wa
taaluma hiyo na kuweza kusaidia vita dhidi ya ubadhirifu wa mali ya umma nchini.
Hivyo ,
Mhe. Othman amewataka watu wote wa jimbo hilo wenye sifa ya kupiga kura
huhakikisha wanajitokeza kwa asilimia mia moja ili kushiriki kumpata mwakilishi
halali wa jimbo hilo mwenye uwezo mkubwa
kitaaluma katika kusaidiana kutimiza malengo ya chama hicho ya kuleta mageuzi
ya kweli ya kidmokrasia na kuchapuza kasi ya vita dhidi ya umasikini Zanzibar.
Amewafahamisha
wananchi hao kwamba Zanzibar inahitaji
kuwepo viongozi makini na majasiri wenye kuacha ubinafsi ambao wataendeleza v
yema mapambano ya kuleta mageuzi ya kweli kisiasa na kimaendeleo unaotokana na
kuendesha nchi kwa msingi ya ukweli na uaminifu miongoni mwa watendaji na
viongozi wenye dhamana mbali mbali.
Amesema
kwamba suala la ufisadi katika nchi halihusishi wizi wan a matumizi mabaya ya
rasilimali za umma pekee b ali pia
kuwepo utaratibu mbaya wa kuendesha nchi kwa misingi ya kukosa uaminifu na
uadilifu jambo ambalo linachangia kuidamirisha nchi kimaendeleo.
Aidha mhe.
Othman ameonya tabia na vitendo vya baadhi ya viongozi kutumia vibaya madaraka
ya umma walioyopewa na kuendeleza ubinafsi
na hivyo kuwatisha kwa kuwalazimisha wapige kura kukichagua chama
wanachokitaka viongozi.
Amesema
kwamba kufanya hivyo mbali na kutumia
madara ya umma vibaya lakini pia ni kosa la jinai ambalo haliwezi kufa na
kuwaonya wanaofanya hivyo kwamba wanaweza kushitakiwa mahakamani hata katika
miaka kadhaa inapopita kwa kuwa sharia za jinai hazina kikomo.
Naye Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama hicho Ismail Jussa Ladhu amewakumbusha wapiga kura hauo
wamba Zanzibar inahitaji viongozi wenye uchungu na nchi yao na wamchaguo Mgombe
wa ACT Wazalendo katika jitiohada za
kweli za kuleta mageuzi ya kimaendeleo .
Naye
Mgombea wa ACT- Wazalendo Dk. Mohammed Ali Suleiman ameama kwamba Jimbo hilo la
Mtambwe ni Jimbo mama katika harakati za mageuzi na kwamba ni muhimu kuendeleza
jitihada za viongozi mbali bali kwa kumchagua yeye kuendeleza jitihada hizo.
Mhe Othman Mapema amefanya mazungunzo na viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo huko Katika Ofisi za ACT- zilizopo Daya Mtambwe, kutembelea na kuzungunza wanabaraza za chama hicho pamoja na kuwajulia hali wagonjwa mbali mbali kisiwani Pemba.
Kitengo cha
Habari
Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Zanzibar.
Oktoba 26,2023
No comments:
Post a Comment