Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo
mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo
Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara
tarehe 14 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo
Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio hizo katika
uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Vijana wa hamasa wakati alipokuwa
akielekea kukagua mabanda ya Maonesho ya Vijana Kitaifa Babati Mkoani Manyara
tarehe 14 Oktoba, 2023.
Matembezi ya Vijana
yakipita mbele ya Jukwaa Kuu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati
Mkoani Manyara
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko pamoja na
viongozi wengine wa Serikali wakati akiangalia Vijana wa Halaiki walipokuwa wakionesha
maumbo mbalimbali uwanjani wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo
Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara
Wakuu wa Mikoa pamoja na
viongozi wengine wakiwa kwenye Sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo
Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara
No comments:
Post a Comment