Habari za Punde

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi yaazimia kuleta maendeleo ya haraka sekta ya uvuvi


Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imepanga mpango mkakati katika kuleta maendeleo ya haraka katika sekta ya uvuvi na mazao ya baharini pamoja na utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

Ameyasema hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt Aboud Suleiman Jumbe huko Jambiani Visitors Inn Hotel wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu juu ya maabara ya kuharakisha matokeo chanya kwa vipaumbele vya ajenda ya uchumi wa buluu(Delivery lab)

Dkt. Aboud amesema kupitia warsha hii kutasaidia kutengeneza mfumo wa uangalizi na kutoa taarifa kwa ajili ya kujenga viashiria ambavyo vitaleta mageuzi ya haraka ya utekelezaji wa vipaombele vya uchumi wa buluu ikiwemo Uvuvi, mwani, uhifadhi, utafiti mazao ya baharini na mafuta na gesi.

Sambamba na hayo Dkt.Aboud amesema sekta ya uvuvi na mazao ya baharini imekuwa kwa kasi kufikia asilimia 6.3 kwa mwaka kutoka asilimia 4.5 kwa mwaka wakati Mheshimiwa Rais akiingia madarakani mwezi wa Novemba mwaka 2020, jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya Uchumi wa Buluu nchini.

Kwa upande wake Meneja wa kushughulikia Uchumi wa Buluu Captain Hamad Bakari Hamad kutoka Taasisi ya Rais ya Kusimamia Utendaji wa kazi Serikalini PDB amesema mashirikiano ya pamoja yanahitajika katika kuisaidia jamii kwa namna zote ili kufikia malengo ya ajenda ya uchumi wa buluu ya kupitia uvuvi mdogo mdogo na ukulima wa mwani katika kila eneo kwa Unguja na Pemba.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema kuwepo kwa warsha hii itasaidia kuweka vipaombele muhimu kwa ajili ya kutekelezeka ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Zanzibar.
Warsha hii imefanyika kwa Mashirikiano ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, WIOMSA, Taasisi ya Rais ya Kusimamia Utendaji wa kazi Serikalini (PDB) pamoja Tony Blair Institute (TBI).

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.