Habari za Punde

Waziri Masoud afunga kozi ya Uongozi

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mh Masoud Ali Mohammed amewataka Wahitimu kuyatumia vyema Mafunzo waliyopatiwa kwa ajili ya kufikiwa Malengo yaliyokusudiwa.
Akifunga kozi ya Uongozi wa kati Sinia Ensio wa mkupuo wa Tisa Chuo cha Uongozi Dunga, amewasisitiza Wahitimu hao Nidhamu, Uzalendo, Amani na Usalama wa Nchi, kiwe kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu ili Nchi ibaki kuwa na Amani na kulinda uhuru.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi JKU, Kanal Makame Abdalla Daima amesema wana jukumu kubwa la kuwapa Mafunzo Askari wao kwa ajili ya kuitumikia Nchi kwa ujumla.
Mkufunzi Mkuu wa chuo hicho Meja Yahya Ali Kondo, amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo wa kiakili na kiubunifu Wahitimu hao, ili kujiweka tayari katika kutumikia taifa kwa Ubunifu na kijiamini.
Akisoma Risala kwa niaba ya Wahitimu hao, Sinia Ensio. Abdulrahaman Mtumwa Madai amesema Mafunzo hayo yatakuwa ni mfano kwa wengine na kuahidi kuyafanyia kazi kwa uzalendo na vitendo.
Miongoni mwa mafunzo waliyopatiwa mawasiliano, Sheria, Uongozi, Uzalendo, Gwaride na Huduma ya kwanza.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.