Habari za Punde

KINANA AWAHAKIKISHIA WANANCHI HANANG MAELEKEZO YA RAIS DK. SAMIA YATATEKELEZWA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, Akitoa pole  kwa baadhi ya Majeruhi Katika Hospitali ya Wilaya hiyo  (Tumaini) iliyopo Katesh, alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wananchi wilayani Hanang Mkoa wa Manyara hususan waliokumbwa na janga la mafuriko, kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu na idara na taasisi zote kama walivyoagizwa chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu

Kinana ameyasema hayo leo Desemba 4, 2023 alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.


Kinana amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu zao na waliojeruhiwa na kulazwa hopitalini kutokana na janga hilo ambapo amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana,akizungumza na Kijana Faustine alipokwenda kutoa  pole  kwa Wakazi wa Kata ya Gendambi alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana,Akiwapa pole Wakazi wa Kata ya Gendambi alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.