Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Ameweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Skuli ya Ghorofa ya Msingi Kojani Pemba,Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Kojani na (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akizungumza  katika hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Msingi Kojani, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Disemba 30, 2023 amehudhuria pia  akiwa Mgeni Rasmi wa Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Jengo la Ghorofa Tatu (3) la Skuli ya Msingi ya Kojani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. 

Hafla hiyo, ambayo ni sehemu ya Shamrashamra kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, imewajumuisha Mawaziri na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini, Jamii, Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Vikundi vya Burudani na Vijana Wahamasishaji  wakiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed Mussa.  

Mheshimiwa Othman yupo kisiwani Pemba kwa Ziara ya Siku Tatu, ikijumuisha pia Uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo, akiwa ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.

Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Disemba 30, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.