Habari za Punde

DKT.PHILIP MPANGO AONGOZA UHAMASISHAJI UPANDAJI MITI KITAIFA ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango akipanda mti aina ya mpilipili doria katika zoezi la uhamasishaji upandaji miti kitaifa lililofanyika taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

Na Khadija Khamis -Maelezo   09/02/2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Mazingira ni  suala mtambuka hivyo ni jukumu la kila  Mtanzania kuiunga mkono Serikali katika utunzaji wa mazingira. 

 

Aliyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji miti katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia katika Chuo cha Karume, Mbweni ikiwa ni ishara ya kuhamasisha upandaji miti Kitaifa.

 

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kutoa elimu na miongozo pamoja na kutunga sera, sheria mbalimbali ili kulipa umuhimu suala hilo juu ya kuhifadhi mazingira .

 

Alifahamisha serikali zote mbili zinashughulikia athari kubwa zinazojitokeza za uharibifu wa mazingira jambo ambalo linachangia mabadiliko ya tabia ya nchi.

 

 “Mabadiliko ya tabia ya nchi yanaathari  kubwa za kusababisha majanga ikiwemo kuongezeka kwa joto nchini, mvua kuwa kubwa na kima cha Bahari kuengezeka na maji chumvi kuingia maeneo ya makaazi ya watu pamoja na kuathiri maeneo ya kilimo ”, alisema Makamu .

 

Dkt. Mpango alizitaka Wizara, Taasisi,Vyuo Vikuu na jamii  kupanda miti kwa wingi kwa lengo la kuiunga mkono serikali na kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya taifa vizazi vijavyo .  

 

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman amesema amefarijika kwa ujio wa kiongozi huyo kwani Ofisi yake kupitia Taasisi ya Mazingira imejipanga kuirudisha Zanzibar katika hali ya kijani na kuongeza haiba nzuri.

 

Alisema kutokana kupotea uhalisia wa kijani serikali inatarajia kuzindua mpango maalumu wa upandaji miti (Green Legal Program) ifikapo tarehe 09 Machi mwaka huu ili kuimarisha mazingira mazuri nchini.

 

Hata hivyo Mhe Harusi alimuomba Mhe.Makamu wa Rais kuweka utamaduni wa kupanda miti kila anapofanya ziara yake Zanzibar ili kuhamasisha jamii juu uhifadhi wa mazingira nchini.

 

Katika zoezi hilo la upandaji miti Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mpango  alipanda mti aina ya Mpilipili doria ambao matunda yake yanakuja kwa wingi na inaleta faida zaidi kwa Zanzibar.



Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Mboni Mpaye akishiriki zoezi la uhamasishaji upandaji miti Kitaifa lililofanyika Taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

Waziri wa Nchi OMKR Mhe .Harusi Said Suleiman akipanda mti katika zoezi la uhamasishaji upandaji miti kitaifa lililofanyika taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar
Waziri wa Nchi (OMPR) Sera, uratibu na Baraza la wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma akipanda mti katika zoezi la uhamasishaji upandaji miti kitaifa lililofanyika taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

Baadhi ya waalikwa wakishiriki zoezi la upandaji miti ikiwa ni uhamasishaji wa zoezi hilo Kitaifa huko Taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

Waziri wa Nchi OMKR Mhe .Harusi Said Sleiman akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango kuhutubia katika zoezi la uhamasishaji upandaji miti kitaifa lililofanyika taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Philip Isdor Mpango akihutubia katika zoezi la uhamasishaji upandaji miti kitaifa lililofanyika Taasisi ya sayansi na teknolojia ya Karume Mbweni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.