Habari za Punde

Benki ya CRDB Yafutarisha Wateja Wao katika Iftari Maalum Iliyowandalia Katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akimkaribisha tende Mufti Mkuu wa Zazibar Sheikh Saleh Omar Kabi kwa ajili ya kufungulia wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B"Unguja Jijini Zanzibar.Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amezitaka Taasisi za Kifedha kufanya ushindani wa kibiashara kwa kutoa huduma bora na zaharaka ambazo zitapelekea kuaminika na kukubalika kwa Serikali na wateja wao.

Ameyasema hayo katika ftari Iliyoandaliwa na Benki ya CRDB iliyofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.

Amesema kuwa Taasisi za kifedha nchini zina mchango mkubwa katika kuinua Uchumi waTaifa na kuchangia katika miradi mbali mbali yakimaendeleo inayoendelea kutekelezwa nchini sambamba na kuwasaidia wananchi mbali mbali katika kuhakikisha wanapata maslahi mazuri kwenye  maisha yao.

Mhe. Hemed ameutaka uongozi wa Benki ya CRDB kuendelea kutoa misaada kwa makundi mbali mbali yenye uhitaji wakiwemo mayatima,wajane, walemavu na watu wasiojiweza kwani kufanya hivyo ni kuunga Mkono jitihada za Serikali za kuhakisha inawaletea maendeleo wananchi wake.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewahakikishia viongozi na wafanya kazi wa Benki ya CRDB kuwa Serikali ya awamu ya nane (8) itaendelaea kutoa ushirikiano na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mashirika na Taasisi za kifedha katika kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amesema kuwa wakati umefika wa kuendana na kasi ya ushindani wa kibiashara kwa kutoa huduma zilizobora na kwa wakati ili kuwarahisishia wateja kupata huduma na kuongeza wateja zaidi pamoja na kulifikia soko la dunia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Afisa Mkuu wa Biasharaoma BOMA RABALLA amesema uongozi wa benk hio utahakikisha unauendeleza utamaduni uliopo wa  kuftari pamoja kati ya watendaji wa Benki  na wateja wao , wadau na makundi mbali mbali ili kujiweka karibu na jamii.

Amesema CRDB inaamini kuwa kujumuika pamoja katika ftari hiyo na matukio mbali mbali ya kijamii ni kuwa  karibu wateja wao sambamba na kuimarisha umoja, upendo na mshikamano  baina yao.

RABALA amesema CRDB mbali na Ftari hio imeamua kutoa  msaada kwa makundi maalum yenye uhitaji ikiwemo kituo cha kulelea watoto cha Amali kulichopo Kinuni na kituo cha zaso kutoka Fuoni Mambo Sasa na kusema kuwa wanaamini msaada huo utawasaidia hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akitoa salamu za Ofisi ya Mufti  Zanzibar sheikh Iddi Hussein Iddi kutoka Ofisi hio amewaasa waislamu kukithirisha ibada pamoja na kutoa sadaka na zaka kwa watu wasiojiweza hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kufikia lengo la kufunga, hivyo amesema Ramadhan ni chuo cha kujifunza Amali njema na kuzidisha kasi ya kufanya ibada na kusoma Qur-an kwa wingi kwa kutarajia kupata radhi za Allah (S.W.S)

Imetolewa na Kitengo cha Habari cha (OMPR)

LEO Tarehe....24.03.2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.