Habari za Punde

Waziri Mhe.Tabia Akagua Eneo Litakalojengwa Ofisi za Magazeti Shirika la Magazeti ya Serikali Tunguu

Waziri wa Habari ,Vijana ,Utamadini na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akipata maelezo kutoka Mhariri Mtendaji Shirika la magazeti ya Serikali Ali Haji Mwadini Mwadini kuhusiana na ujenzi wa ofisi za shirika hilo huko Tunguu Wilaya ya kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Waziri wa Habari ,Vijana ,Utamadini na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akikagua eneo linalotarajiwa kujengwa Ofisi za Shirika la magazeti ya Serikali huko Tunguu Wilaya ya kati , Mkoa wa Kusini Unguja.

Na Sheha Sheha.

Zaidi ya shilingi bilioni 8 zinatarajiwa kutumika katika Ujenzi wa ofisi za shirika la Mageziti ya Serikali.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita mara baada ya kufanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa Ofisi hizo huko Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Waziri Tabia alisema licha ya shirika hilo kutanuka kiutendaji lakini bado kumekuwa na changamoto za mazingira ya kufanyia kazi hivyo Mradi wa ujenzi huo utachangia ubora katika utendaji wa Shirika hilo.

“Kwakweli Shirika la Magazeti linahitaji ofisi kubwa kwa sababu tumetanua mawanda yetu lakini hata mauzo ya magazeti pamoja na kusambaza magazeti Tanzania nzima"alisema.

Amesema, ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu hivyo amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuwa wastahamilivu katika kazi zao hadi utakapokamilika ujenzi huo ambao utawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amefahamisha kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutachangia kuongezeka kwa uzalishaji wa Shirika hilo hali ambayo itawasiaidia wafanyakazi kuboreshewa maslahi yao.

Nae Muhariri Mtendaji  wa Shirika hilo Ali Haji Mwadin amesema ujenzi huo unatarajiwa kujengwa awamu kwa awamu hadi  kukamilika ndani ya miaka miwili.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.