Habari za Punde

Kuhitimisha zaiara zake za kuwatembelea wagonjwa katika mikoa yote unguja na pemba

Na.Mwandishi OMWR. 

Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba amewataka viongozi wa chama hicho katika ngazi mbali  mbali kujitahidi kuwa sauti ya wananchi kwa kuibua ip[asavyo matatizo mbali mbali yananayowakabuili na kuyawasilisha ili serikali iweze kuchukua hatua.

Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo huko Shakani wilaya ya Magharibi B Unguja alipofanya majumuisho ya ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa, vizuka na wenye shida mbali mbali ikiwa ni utaratibu wa chama hicho uliowekwa na mtangulizi wake marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Mhe . Othman amefahamisha kwamba katika ziara hiyo ameweza kushuhudia mambo na matatizo  na changamoto kadhaa ya wananchi ambayo amejifunbza kwamba yanahitaji kusimamiwa na viongozi katika ngazi mbali mbali  hasa kutokana na kuona kwamba ameweza kujifunza kwamba wapo wananchi wengi ambao wanaishi katika maisha duni sana

Amesema kwamba ni wajubu wa viongozi kushriikiana ili kuona kwamba matatizo ya wananchi walionayo wanajitahidi kuandaa mikakati na mipango mbali mbali iliyosahihi na madhubudi na kufanya kazi ya kuwa sauti ya wananchi katika kuzifikia na kuzitatua changamoto za wananchi zinazowakabili katika maeneo yao wanayoishi.

Amesema pia ameweza kujifunza na kushuhudia  shida na changamoto za wananchi zilizopo katika maisha yao ya kila siku ambazo nyengine, sio kwamba zimeshindikana kutatuliwa, lakini  inatokana na baadhi ya watendaji kutokujali na kufanya kazi zao kwa kuwajibika kwa umakini katika kuzikabilki shida hizo.

Amewataja waatendaji hao kuwa  ni katika ngazi mbali mbali za serikali za mitaa , shehia na serikali kuu ambapo ingewezekana kuchukuliwa hatua kwa matatizo ambnayo wananchi wanakabiliana nayo na kuweza kutatutuliwa.

Aidha Mhe. Othman amasema kwamba hivi sasa Zanzibar wananchi wanaendelea  kukumbwa na  tatizo kubwa la  maradhi yasioyoambukiza yakiwemo changamoto ya sukari, mgongo na mifupa pamoja na kupooza jambo ambalo ni maradhi yanahitaji kinga zaidi kuliko tiba.

Amesema kwamba maradhi haya yanahitaji kinga zaidi,  lakini pia yanapotokea bado matibabu yake ni changamoto zaidi kwa wananchi hasa katika utumiaji wa dawa kwa kuzingatia utaratibu sahihi kama inavyoelekezwa na wataalamu ili kuwa na uhakika wa kukabiliana na maradhi hayo ipasavyo.

Naye Mwekiti wa Chama hicho katika Mkoa wa Magharib B Kichama Ali Juma amesema kwamba Zanzibar inaendelea kuwa na umasikini ambao unaweza ,kuondolewa kwa kuwepo juhudi za pamoja na wazanzibari kuendelea kuishi vyema.

Aidha wamempongeza mwenyekiti huyo kutokana kufanya ziara hiyo katika mikoa yote 11 kichama na kutekeleza majukumu yake mbali mbali kwa ufanisi mkubwa kulingana na malengo ya chama hicho

Mhe. Othman tayari amekamilisha ziara hizo katika Mkoa wa Kusini Unguja, Mjini Magharib na mikoa miwili ya Pemba ambapo leo amekamilisha ziara yake hiyo katika wilaya ya Magharib A na B.

Ziara hizo ni mwendelezo wa urithi uliachwa na Mtangulizi wake Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad ambazo  katika uhai wake alizifanya kila ifikapo mwenzi mtukufu wa Ramadhani kuwatembelea wagonjwa, wenye misiba na shida nyeingine mbali mbali katika visiwa vya Unguja na Pemba.

 Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Kitengo chake cha habari leo Jumatano tarehe 27 Machi 2024.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.