RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea
salama za pole kutoka kwa kampuni ya WASAFI inayoongozwa na Mkurugenzi mkuu,
Nasib Abdul (Dimond Platinum)
Dk. Mwinyi
alipokea Salamu hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na kiongozi huyo na
ujumbe aliofuatana nao.
Rais Dk.
Mwinyi aliushukuru uongozi wa Wasafi uliofika kwa lengo la kumfariji kufuatia
msiba wa Baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Mzee Ali Hassani Mwinyi aliyefariki Februari 29, 2024, Dar es
Salaam na kuzikwa Kijiji cha Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja, Machi, 02
mwaka huu.
Pamoja na
mambo mengine pia, Rais Dk. Mwinyi pia aliwashukuru Wasafi kwa kujitoa kwako na
kuungamkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyatangaza mazuri
yote yanayofanywa na serikali kupitia Sanaa yao ya muziki.
Naye, Dimond
Platinum amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada zake za kuendelea kuwaletea maendeleo
makubwa wananchi wa Zanzibar na kusifia jitihada zake wamekua wakizishuhudia
kila uchao kupitia mafanikio makubwa kwenye huduma za jamii ikiwemo sekta ya
Elimu na Afya.
Alisema
hatua za maendeleo zilizofikiwa na Serikali ya Rais Dk. Mwinyi zimevuka malengo
ya Ilani ya CCM na Kwenda mbali zaidi.
Dimond
Platinum ni nyota maarufu wa Sanaa ya muziki wa “bongo Flavor” Tanzania pia ni
mwanamuziki aliefanikiwa kuliteka soko la muziki wa kisasa Afika Mashariki,
Afrika na dunia kwa ujumla.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment