Kwanza tunashukuru sana Mwenyenzi Mungu kwa kutukutanisha tena na katika mwezi huu mtukufu na wa fadhila nyingi, tukiwa tuko hai na wazima.
La pili, sisi watekelezaji
wa mradi wa kuwezesha wanawake na jamii kudai haki zao za kidemokrasia na
uongozi (SWIL), ZAFELA, PEGAO na TAMWA ZNZ tunapenda kutoa shukurani zatu za
dhati kwa wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za kiserikali, taasisi za kijamii,
jamii, waandishi wa habari, wahamasishaji jamii, viongozi wa dini na taasisi
binafsi ambao wamekua nasi pamoja katika utekelezaji wa mradi wa ambao ulianza
utekelezaji wake mwaka 2020 hadi na kumalizika mwaka jana 2023.
Kupitia mikutano ya kijamii
tumeweza kufikia jumla ya jumla ya watu 11, 129 wengi wakiwa ni wanawake katika
mikoa yote ya Zanzibar kupitia mikutano ya uhamasishaji, majadiliano,
ufuatiliaji na mafunzo mbali mbali.
Pia mradi umewawezesha
wanawake 200 ambao walijengewa uwezo kuhusu masuala ya kidemokrasia, siasa, na
uongozi ili waweze kushiriki katika vyombo vya maamuzi.
Aidha, jumla ya waandishi
wa habari 199 wamejengewa uwezo wa kuandika habari zinazogusa masuala muhimu
kuhusu haki za wanawake na jamii, ambapo jumla ya habari 2,127 ziliandikwa
kupitia radio, magazeti na mitandao ya kijamii na kuibua mijadala na kuchochea
uwajibikaji wa taasisi mbalimbali ambazo zilisaidia kuleta matokeo chanya
katika jamii.
Tumepitia sheria mbali
mbali pamoja na Sheria ya Kadhi 2017,
Sheria ya utumishi wa umma (kushiriki katika siasa) No.03 2003, Sheria ya
Baraza la Vijana No.16 2013, Sheria ya uchaguzi No. 4 2018, sera ya jinsia ya
Tume ya Uchaguzi, Sheria ya utumishi wa umma 2011, Sheria ya vyama vya siasa
CAP 258 2002 na Sheria ya Tawala za Mikoa chaNo.7 2014.
Tumeweza kukutana na
wahusika mbali mbali wakiwemo Serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyombo
vya habari ili kuomba mabadilko ya sera, miongozo, utendaji na uwajibikaji.
Mradi huu ulilenga
kumuwezesha mwanamke ambapo ili siyo tu awe kiongozi lakini awe kiongozi bora.
Kwa hivyo, tuliweza kuwasimamia ili waweze kufikia lengo hilo ikiwemo pia
kuwafundisha sera na haki zao na kuweza kufuatilia haki zao binafsi na haki za
wanajamii. Hii tuliifanya kupitia Wahamasishaji jamii (CBs), ambao walijengewa
uwezo katika masuala ya uongozi, siasa na Kwa hivyo, waliweza kuibua changamoto zaidi ya 1,000 za jamii na za mtu
mmoja mmoja. Zaidi ya changamoto 771 wameweza kuzichukuliwa hatua na zaidi ya
400 zimeshapatiwa ufumbuzi.
Waandishi wa habari kwa upande wao waliibua
viongozi mbali mbali, waliibua maswali mbali mbali. Kwa mfano Nihifadhi
….aliandika habari kuhsusu bi Njuma Ali Juma wa Meli NNe SACCOSS alivyoanzisha
na kuipaisha SACCOSS hiyo hadi kuwa na magari yake wenyewe na kutoa mkopo hadi
milioni 10.
Mwandishi Khadija Kombo aliandika habari
kuhusu muwekekezaji aliyeweka ukuta Michamvi ambapo watu walishindwa kupita na
jitihada za wananchi kumkataza ziligonga mwamba. Baada ya kipindi chake
kulichotoka kwenye televisheni Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja aliingia kati na
kumshauri muwekezaji huyo kuvunja ukuta huo.
Tumeweza kuandaa pia sera
ya kijnsia , madawati ya kijinsia na taarifa katika vyombo vya habari 11
ambavyo hadi sasa vyombo saba vimeshapitisha sera zake.
Tunashukuru pia tumeaandaa
tunzo za umahiri kwa wandishi wa Habari na tumekuwa tukipata washindi. Jumla ya washindi 35 walipatikana ambapo
kati yao wanawake walikua ni 29 na wanaume 6.
Tunatoa Pongezi za dhati
kwa Mamlaka za uteuzi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa
kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo hivyo kuongeza idadi ya
viongozi wanawake katika kipindi chake uongozi.
Sno |
Leadership Position |
Men |
Women |
Total |
%age of Women |
1 |
Ministers |
12 |
6 |
18 |
33% |
2 |
Deputy Ministers |
4 |
3 |
7 |
43% |
3 |
Principal Secretaries (PS) |
11 |
7 |
18 |
39% |
4 |
Deputy Principal Secretaries (DPS) |
7 |
5 |
12 |
42% |
5 |
Regional Commissioners (RC) |
4 |
1 |
5 |
20% |
6 |
Regional Administrative Secretaries (RAS) |
4 |
1 |
5 |
20% |
7 |
District Commissioners (DC) |
8 |
3 |
11 |
43% |
8 |
Judges |
7 |
4 |
11 |
36% |
9 |
Shehas |
325 |
66 |
391 |
17% |
|
TOTAL |
383 |
95 |
478 |
|
Pia katika vyama tumeona
mashirikiano na vyama vya siasa, CCM, chama cha ACT kimeandaa sera ya kijinsia
na hivyo kuwa na malengo ya kuleta usawa wa kijinsia katika chama.
Hata hivyo, mradi
ulikumbana na changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na upatikanaji mdogo wa
takwimu za nafasi za wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi, kukosekana
kwa sera na sheria zinazolazimisha usawa wa kijinsia katika sekta zote, baadhi
ya viongozi hawazingatii usawa wa kijinsia katika teuzi mbalimbali
wanazozifanya pamoja na kukosekana kwa sera ya jinsia katika vyama vya siasa.
Vilevile, mifumo ya
upatikanaji wa haki saa nyengine inakuwa ni kikwazo kwa wananchi kupata huduma
kwa urahisi. Kwa mfano wale ambao hawana vyeti vya kuzaliwa Pemba.
Kubwa pia ni ukosefu wa
kanzi data za wanawake na uongozi kaitka ngazi zote kwa mfano viongozi wa Bodi,
wajumbe taasisi binafsi, na data base ya wanawake wanaoweza kuwa viongozi.
Katika kipindi cha
utekelezaji wa mradi, tumejifunza umuhimu wa kutumia vyombo vya habari katika
kupaza sauti za jamii katika kuibua changamoto zao na kuongeza uwajibikaji wa
viongozi, muamko wa elimu kwa wanawake
kuhusu haki zao umeonyesha kuwa unawezesha
kudai na kufuatilia haki zao na Ushirikiano na wadau mbalimbali
umethibitisha kuwa muhimu katika kufanikisha malengo ya kijamii.
Kwa kuzingatia
yaliyojifunza na mafanikio yaliyopatikana, tunapendekeza yafuatayo:
1. Kuanzishwa kwa kanzidata
ya viongozi wanawake waliyoko katika sekta mbalimbali.
2. Kuweko kwa sera na
sheria zinazolazimisha usawa wa kijinsia katika sekta zote.
3. Kuwepo kwa mifumo rafiki
ya upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Mwisho, si kwa umuhimu
tunatoa shukurani kwa ubalozi wa Norway nchini Tanzania kwa kufanikisha
utekelezaji wa mradi huu, na tunatoa
wito kwa wadau wote wa maendeleo kushirikiana katika kuwawezesha wanawake na
jamii kwa ujumla kudai haki zao za kidemokrasia, siasa, na uongozi.
Imetolewa na:
Chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ)
Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar
(ZAFELA)
Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba
(PEGAO)
Na KUSOMWA NA Dkt. MZURI
ISSA,
MKURUGENZI TAMWA,ZNZ.
No comments:
Post a Comment