Habari za Punde

Mapato ya Bandarini yamepanda asema Dkt. Khalid.

Na Takdir Ali.Maelezo. 12.05.2024.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na uchukuzi Zanzzibar Mhe.Dkt Khalid Salum Mohamed amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii ya kuwa mapato ya Bandari ya Zanzibar yameshuka kwa asilimia 95  mara baada ya kupewe muwekezaji wa Zanzibar MultipurposeTerminal (ZMT).

Amesema kauli hizo hazina ukweli wowote na sinapaswa kupuuzwa na jamii kwani haijapata kushuka mapato kwa kiasi hicho hata kabla ya kupewa muekezaji huyo.

Dkt.Khalid ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusiana na taarifa hizo potofu.

Amesema tokea kupewa muekezaji huyo Bandari imeimarika sana na Mabato yameongezeka kwa kiasi kkubwa. 

Amesema hali ya udhibiti wa uingiaji na utokaji umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuingia kwa shughuli maalum na vitambulisho maalum.

"Watu ilikuwa wanaingia na kutoka bila ya mpangilio wowote lakini sasa hivi tunaona , ZMT imefanya kazi kubwa kudhibiti watu na sasa kwa shughuli maalum huku wakiwa na vitambulisho maalum."alisema Dkt. Khalid.

Aidha amesema hali ya usalama imeimarika baada ya muwekezaji huyo kuweka taa katika sehemu ya Bandari jambo ambalo litasaidia kuondosha udanganyifu na upotevu wa mapato.

Amefahamisha kuwa muwekezaji huyo pia amechukuwa wafanya kazi zaidi ya elfu 3 (300,000) waliokuwa wakifanya kazi sehemu ya bandari, ametengeza ajira mpya kiasi ya 40 na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi hao jambo ambalo limeongeza ufanisi wa kazi na usalama.

Samamba na hayo amesema miongoni mwa sharti alilopewa katika mkataba wake ni kuongeza eneo katika kufanyia shughuli za bandari ambapo alipewa hekta mbili katika eneo la maruhubi kwa muda wa miezi 4 na tayari ameshafanya kazi kwa asilimia 50 na itakapofika July itakuwa ameshakamilisha kwa asilimia 100.

Mbali na hayo Dkt. Khalid amewataka kufuatilia taarifa zinazotolewa katika vyanzo husika ili kujiiepusha na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.