Habari za Punde

Mzumbe Yafanya Udahili wa Moja kwa Moja katika Maonesho -- TANGA

1. Wageni mbalimbali waliotembelea maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu wakipata huduma kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe.

Chuo Kikuu Mzumbe kimewataka wahitimu wa Sekondari na waombaji wengine wanaotaka kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada za Umahiri na Shahada za Uzamivu kuchangamkia fursa ya usajili inayotolewa katika Banda la Chuo hicho, kwenye maonesho ya  wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari  Popatlal  kuanzia Mei 25 hadi Mei 31, 2024.

Mkuu  wa Idara ya Udahili  Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt Michael Mangula amesema  dirisha la uhadili limeshafunguliwa  kwa kozi mbalimbali zinazofundishwa na Chuo Kikuu Mzumbe  zikiwemo Masomo ya biashara, sheria , teknolojia ya habari na mawasiliano, Uchumi, Manejimenti  utawala, uhasibu ,ujasiliamali , ualimu na, utawala katika afya na nyingine nyingi. 

Amesema wananchi wanayo fursa ya kufanya udahili wa hapo kwa hapo kwa njia ya mtandao (online registration)  katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho ya wiki ya  Elimu, Ujuzi na Ubunifu  au kufika katika Kampasi za chuo mkoani Morogoro, Mbeya au Dar es salaam Upanga na Tegeta kwa Ndevu kwa mwaka wa masomo 2024/2025 utakaoanza Oktoba mwaka huu. 

Aidha Mkuu huyo wa Idara ameongeza kuwa kutokana na kufunguliwa kwa dirisha la udahili, popote mwombaji alipo anaweza kujisajili kwa njia ya mtandao, na kwamba anawasihi waombaji kutembelea tovuti ya chuo ya admission.mzumbe.ac.tz/ au www.mzumbe.ac.tz kwa taarifa zaidi kuhusu kozi na taratibu zingine za kujiunga. 

Amewasisitiza wananchi wa jiji la Tanga kuchamkia fursa ya kujiendeleza kielimu kupitia chuo kikuu mzumbe  kwani tayari chuo hicho kimepata eneo Wilayani Mkinga kwa jili ya kujenga  Kampasi ambapo masomo ya cheti, diploma na shahada za awali yatafundhishwa.


 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Mzumbe Bi. Lulu Mussa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliotembelea na kuhudumiwa kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe  wakati wa maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu

    Mkuu wa kitengo cha ununuzi Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Castor Komba akikabidhiwa zawadi ya kumbukumbu baada ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za kike Ndaki ya Mbeya. Bw. Komba alikabidhiwa zawadi hiyo alipotembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa maadhimisho ya wiki ya  kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu.


Wageni mbalimbali waliotembelea maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu wakipata huduma kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.