Habari za Punde

Wadau wa Masuala Takwimu Wakutana Kujadili Changamoto za Watoto

Naibu Katibu Mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Khatibu Mwadin Khatib  akifunguwa mkutano wa robo mwaka wa Jukwaa Jumuishi la mashauriano, uratibu na ufuatiliaji wa mambo yanayokwamisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na Watoto huko ukumbi wa Zura Maisara Zanziabr.

Na Takdir Ali. Maelezo. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Khatib Mwadin Khatib amesema suala la takwimu ni muhimu katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji.

 

Ameyasema hayo huko katika ukumbi wa ZURA Maisara wakati alipokuwa akifunguwa mkutano wa robo mwaka wa Jukwaa Jumuishi la mashauriano, uratibu na ufuatiliaji wa mambo yanayokwamisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na Watoto.

 

Amesema bila ya takwimu hawatoweza kujuwa makosa yao na kupata njia mbalimbali za kuondosha vitendo hivyo.

 

Aidha amewataka kuzihifadhi na kuzisambaza kwa wanaohusika ili wapate mchanganuo sahihi na kuzifanyia kazi takwimu hizo.

 

Hata hivyo amesema Wizara imepanga mikakati mbalimbali ikiwemo utayarishaji wa mpango Mkakati mpya wa kitaifa wa kutokomeza vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na Watoto.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya jamii, jinsia na Watoto Siti Abasi Ali wameweka uataratibu wa kukutana kila baada ya miezi 3 ili kuweza kufikia malengo kumlinda mtoto kutokana na udhalilishaji na ukatili.

 

Amesema masuala ya mapambano yanahitaji nguvu za pamoja ili kuweza kushinda hivyo wasivunjike moyo waendelee kushikamana na kuwa kitu kimoja.

 

Kwa upande wake Ali Haji Hamad Afisa program za jinsia kutoka Shirika la Umoja wa mataifa la Idadi ya watu (UNFPA) amesema lengo la kukutana baraza la mashauriano la mtoto ni kujadili mapungufu na changamoto zilizopo na kuweza kuzifanyia kazi ili kuleta ustawi nzuri kwa Watoto.

 

Aidha ameziomba Taasisi kuzidi kushirikiana kutoa michango yao yah ali na mali ikiwemo fedha ili kuendesha mapamabano ya kupinga udhalilishaji wa wanawake na Watoto katika jamii.

 

Mkutano huo wa jukwaa la Mashauriano Uratibu na Ufuatiliaji wa mambo yanayokwambisha mwitikio dhidi ya wanawake na Watoto na ndoa za utatoni umewashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi, Madawati ya kijinsi, Dpp na Mahakimu wa Mahakama zinazoshughulikia masuala ya udhalilishaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.