Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Nchemba Azungumza na Rais wa China Exim Bank

                                         

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiongoza ujumbe wa Wizara yake wakati wa mkutano na Rais wa Benki ya Exim ya China, Bw. Ren Shengiun (hayupo pichani) uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma ambapo walijadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Rais wa China Exim Bank, Bw. Ren Shengiun (katikati) akieleza utayari wa Benki yake kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kushiriki katika kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akifuatilia maelezo ya Rais wa Exim Bank-China, Bw. Ren Shengiun (hayupo pichani) wakati wa mkutano kwa njia ya mtandao jijini Dodoma na Rais huyo ambapo walijadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo pamoja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Amina Khamis Shaaban na Kulia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya mkutano kwa njia ya mtandao kutoka jijini Dodoma na Rais wa China Exim Bank, Bw. Ren Shengiun, ambapo wamejadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, DKT. Nchemba, ameiomba Benki hiyo kusaidia upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya nchi kwa sasa.

 

Kwa upande wa Tanzania Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Bw. Rished Bade na Kamishna Msaidizi wa Usimamizi wa Madeni, Bi. Tiba Kisonga na maafisa wengine wa Wizara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.