Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga baada ya kuzungumza katika Tamasha la Kizimkazi lililolenga kukuza Utalii Zanzibar, ambalo lilifanyika katika uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar, Agosti 21, 2024.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama ngoma katika Tamasha la Kizimkazi lililolenga kukuza Utalii Zanzibar, ambalo lilifanyika katika uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar, Agosti 21, 2024. Wa tatu kulia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadan Soraga, wa pili kushoto ni Naibu Waziri Utamaduni , Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Maalim Mahfoudhi
Wasanii wa kikundi cha Motomoto wakitumbuiza katika Tamasha la Kizimkazi lililofanyika kwenye uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar, Agosti 21, 2024. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Wasanii wakicheza ngoma ya Lizombe katika Tamasha la Kizimkazi lililolenga kukuza utalii visiwani Zanzibar ambalo lililofanyika kwenye uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar, Agosti 21, 2024. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Tamasha la Kizimkazi lililolenga kukuza Utalii Zanzibar, ambalo lilifanyika katika uwanja wa Shekha Dimbani, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment