Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Amekutana na Uongozi wa D-TREE

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano na mashirikali mbali mbali ya kimataifa katika kuwaletea maendeleo wanachi wake ikiwemo kuimarisha afya ya mama na mtoto kwa maslahi mapana ya wananchi wa unguja na pemba.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Uongozi wa Shirika la Kimataifa la D- TREE ( Dtree International ) ambalo linafanya kazi zake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar hasa kwenye huduma za afya ya jamii waliofika ofisini kwake vuga kwa lengo la kujitambulisha.

Amesema kuwa serikali itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwa shirika hilo ili liweze kufanya kazi zake  kwa ufanisi katika kuwapatia elimu wafanya kazi wa Afya hasa wale wa vijijini ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa kila mwananchi.

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar amesema kuwa mpango (program) waliyokuja nao Shirika hilo wa kuwapatia   elimu wafanyakazi wa kujitolea ( CHV) katika sekata ya afya utasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga hatua za kimaendelea kwa sekta hio kwa maslahi mapana ya wananchi wa Unguja na Pemba.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kuwapa kipao mbele wafanya kazi wanaojitolea katika Sekta ya Afya ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi hasa wale wa vijijini ikiwemo kutoa elimu ya kujikinga na maradhi yasio ya kuambukiza kama vile kisukari, pressure na mengineyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji Shirika la kimataifa la D- tree Zanzibar RICCARDO LAMPARIOLA ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwaamini na kufanya nao kazi hasa katika huduma za Afya ya jamii kwa maslahi mapana ya wananchi wa Zanzibar.

Amesema  kwa sasa shirika lao limekuja na program ya kufanya kazi zao kwa njia ya Kijiditali ambayo itawasaidia wafanyakazi wa sekta ya Afya hasa wale waanojitolea ( CHV ) kufanya kazi zao kwa urahisi na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi wote.

Aidha bwana RICCARDO amesema kwa kushirikiana na jamii ya wazanzibari anaamini malengo ya Shirika lao ya kutoa huduma zilizobora kwa wafanyakazi wa huduma za Afya kwa Wilaya zote za Unguja na Pemba yataweza kufikiwa kwa ufanisi zaidi.

 

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.