KUSINI, PEMBA
07 OKTOBA,
2024
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameziagiza
taasisi zote zinazotoa huduma za usatawi kwa Wazee, kuzishughulikia haraka na
kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili Wazee hao.
Dk.
Mwinyi ametoa maagizo hayo ukumbi
wa ZSSF, Tibirinzi Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini, Pemba kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya Wazee, duniani.
Taasisi
zilizopewa maagizo hayo ni Wizara ya Afya kuagizwa kuandaa madirisha maalumu
hospitali zote ya kutoa huduma za Wazee kwa kuwapa kipaumbele, pamoja na
kuongeza madaktari bingwa wa magonjwa ya wazee.
Rais
Dk. Mwinyi pia ameziagiza Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kuishughulikia
Sheria vya vyombo vya barabarani na kuharakisha mchakato wa kuwapatia Wazee
vitambulisho maalumu vitakavyowasaidia kulipa nusu nauli kama ilivyo kwa
wanafunzi na watu wenyeulemavu.
Aidha,
Wizara ya Fedha imeagizwa kuandaa bajeti maalumu ya kuendesha mabaraza ya Wazee
pamoja na kufungua madirisha maalumu kwenye benki na huduma za Fedha
yatakayotoa msaada na kipaumbele kwa kuwahudumia Wazee hao.
Halikadhalika,
Rais Dk. Mwinyi ameitaka Wizara ya Wanawake, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana taasisi na jumuiya
zinazoshughulika na masuala ya Wazee nchini kuendelea kutoa elimu kwa jamii
kuepukana na mitazamo potofu kwa kuwapachika wazee tuhuma za uchawi.
Rais Dk. Mwinyi amesema, Serikali imeandaa na inaendelea
kutekeleza Sera ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2014 ambayo imeweka mikakati
madhubuti ya kusimamia maendeleo ya Wazee.
Ameeleza kuwa, Serikali imetunga Sheria ya
Masuala ya Wazee nambari 2 ya
mwaka
2020 kwa maadhimisho ya kusimamia haki na maslahi ya wazee nchini.
Dk. Mwinyi amesema, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Jumuiya na Mabaraza ya
Wazee katika ngazi za Mkoa, Wilaya na
Shehia inafanya kila juhudi kusimamia na kuimarisha maendeleo ya Wazee nchini.
Alisema
hadi sasa shehia na Wilaya zote nchini wameshaanzisha mabaraza ya Wazee. Kwa
hakika, hii ni hatua kubwa kwani mfumo huu wa kuwepo mabaraza kuanzia ngazi ya
chini kabisa unasaidia katika kupeleka taarifa kwa wepesi na kurahisisha
utatuzi wa changamoto pale zinapotokezea.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya
siku ya Wazee duniani, Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma amesema Serikali ya Mapindizi
ya Zanzibar itaendelea kuwapa Wazee maisha yenye heshima kama wanavyotambulika
kwenye katiba zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar.
Akisoma
risala kwa niaba ya Wazee wenziwe, mwakilishi wa Wazee, Ali Said Mattar
ameiomba Serikali kuwapa kipaumbele Wazee kwenye huduma za Afya, usafiri, na
benki kwa kuwaharakishia mchakato wa kuwapatia vitambulisho maalumu
vitakavyowatambulisha sehemu hizo pamoja na kuwapatia nafasi maalumu za
uwakilishi kwenye vyombo vya kutungia Sheria ikiwemo Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Baraza wa Wawakilishi ili kuzisemea changamoto
zinazowakabili.
Aidha,
Wazee hao wameiomba Serikali kuifanyia marekebisho Sheria ya usafiri wa vyombo
vya barabarani, Sheria namba 07 ya mwaka 2007 kwa kuwatoza nusu nauli wazee
wote kwenye usafiri wa umma kama ilivyo kwa wanafunzi na watu wenye ulemavu.
Pia wamempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kuwaongezea Wazee pensheni Jamii kutoka
elfu 20 hadi 50 na pensheni ya wastaafu kutoka elfu 90 hadi laki moja na 80.
Naye,
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa "HelpAge" Smart Smart
Daniel, ameisifu Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwajali,
kiwathamini na kuwatunza Wazee kwa kutumia gharama kubwa zaidi ya bilioni 17. 6
kwaajili ya kulipia pensheni Jamii suala alilosema kuwa Zanzibar ni nchi ya
kwanza duniani kwa Serikali kutumia gharama kubwa kwa Wazee bila ya misaada
kutoka nje au mashirika ya kimataifa.
Siku
ya Wazee duniani ilianza kuazimishwa mwaka 1991 na Tanzania hususani Zanzibar
ilianza mwaka 2004 na ujumbe mahususi Kila mwaka, ambapo ujumbe wa mwaka huu ni
"KUZEEKA KWA HESHIMA; UMUHIMU WA
KUIMARISHA MATUNZO NA MIFUMO YA USAIDIZI KWA WAZEE"
IDARA
YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment