Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongoza kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Biashara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan Juma, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Salhina Mwita Ameir.
Mawaziri
kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakishiriki kikao cha Kamati ya
Pamoja ya Fedha na Uchumi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT)
na SMZ kilichofanyika jijini Dodoma kuanzia kushoto Waziri wa Nchi Ofisi Rais
(Fedha na Mipango) Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya
Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) akishiriki kikao cha
Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi SJMT na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.
Wengine kuanzia kulia ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe na Naibu Waziri wa Uchukuzi
Mhe. David Kihenzile.
Naibu Makatibu Wakuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili kulia ni Bw. Abdallah Hassan Mitawi (Muungano) na Bi. Christina Mndeme wakifuatilia kikao cha Kamati ya Pamoja ya Fedha na Uchumi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo.
No comments:
Post a Comment