RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza
Mabalozi wa Nchi za Afrika wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, kuimarisha
ushirikiano na fursa za kiuchumi pamoja na kuutangaza Utalii wa Zanzibar
Kimataifa.
Dk.
Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na mabalozi hao waliofika Ikulu baada ya
kumaliza ziara yao ya siku tatu kuitembelea Zanzibar kuangalia fursa za
uwekezaji na maeneo ya ushirikiano ambayo nchi hizo za Afrika zinaweza
kufanyakazi kwa pamoja na Zanzibar.
Rais
Dk. Mwinyi amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuungana mkono na
kuzitumia rasilimali tulizonazo kuinua Uchumi wetu, kubadilishana uzoefu ili
kufikia maendeleo.
Alisema,
Zanzibar ina utajiri mkubwa wa viungo na fukwe nyeupe zenye kuvutia na
kuwasisistiza kuwa mabalozi wa utali wa Zanzibar na kuitangaza ili watalii
kutoka katika nchi zao kuja kutalii Zanzibar.
Dk.
Mwinyi amewaeleza mabalozi hao kuangalia fursa za ushirikiano na uwekezaji hasa
katika sekta za utalii, Usafiri wa bahari na usafirishaji, Uvuvi na ufugaji wa
vifaranga vya Samaki, Mafuta na Gesi na kilimo cha viungo ambacho Zanzibar kina
utajiri mkubwa.
Kuhusu
sekta ya utalii, Dk. Mwinyi ameuelezea ni tegemeo kwa uchumi wa nchi
unaochangia asilimia 30 ya pato la taifa mbali na kutangaza utalii wa fukwe na
Urithi lakini pia aliwataka mabalozi hao kuangalia fursa mpya za utalii wa
mikutano na uwekezaji ili kuitangaza
zaidi Zanzibar iingize watalii wengi kutoka maeneo mengine ya dunia.
Akizungumzia
Sekta ya usafiri wa bahari na usafirishaji, amewaeleza mabalozi hao kuangalia
fursa zinazopatikana kwenye Sekta hiyo kwa kuziunganisha nchi za Afrika zilizo
katika ukanda wa bahari ya Hindi kwani kwa pamoja nchi hizo zinauwezo wa
kufanya biashara kubwa iwapo sekta hiyo itaimarishwa.
Kuhusu
sekta ya Uvuvi na ufugaji wa Samaki Rais Dk. Mwinyi aliwataka mabalozi hao
kuiungamkono Zanzibar na kuipatia uzoefu uliopo kwenye nchi zao ili inufaike na
uzalishaji wa bidhaa za baharini.
Akizungumzia
suala la Mafuta na Gesi amewaeleza mabalozi hao kwamba Zanzibar imebaini kuwa
na kiwango kikubwa cha gesi na tayari imeanza mchakato wa kugawa vitalu
kwaajili ya kuvuna rasilimali hiyo.
Amesema,
ili kuimarisha sekta ya utalii iendelee kufanya vizuri zaidi, Serikali
inaendeleza juhudi za kuendeleza ujenzi wa miundombinu ikiwemo viwanja vya
ndege Unguja na Pemba, bandari na barabara za kisasa ili kurahisisha sekta ya
usafirishaji na kuwavutia wageni wanaoingia nchini.
Wakizungumza
kwenye hafla hiyo mabalozi hao wamesifu mabadiliko makubwa ya maendeleo katika
kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Dk. Mwinyi, husuasa kwenye ujenzi wa
Miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na bandari pamoja na hali ya amani
na utulivu uliopo nchini.
Balozi
kiongozi wa ujumbe huo, Dk. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema wakati umefika
kwa balozi za Afrika kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali hasa ya kiuchumi.
Pia,
ameielezea Zanzibar kuwa na fursa nyingi zinazoweza kutumiwa na nchi za Afrika
kunufaika nazo kiuchumi na kumuhakikisha Rais Dk. Mwinyi wanakwenda kuutangaza
utalii wa Zanzibar katika nchi zao na kuwa na ushirikiano wa maslahi ya pande
zote.
Naye,
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Issack Jenga Nchi za Afrika zinaweza kuinuana
na kushirikiana zenyewe kiuchumi, hatua itakayosaidia kukwepa misaada yenye
masharti magumu kutoka kwenye nchi zilizoendelea.
Amesema
watatumia fursa ya uwepo wao Zanzibar na kuutangaza utalii wa Zanzbad na
kutimiza ndoto ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikubwa cha utalii unaovuitia
duniani.
Ujumbe
huo wa mabalozi kutoka nchi za Burundi, Comoro, Kenya, Malawi, Misri, Morocco,
Sudan, Rwanda, Uganda na Zambia, ulifika Ikulu ukiongozwa na Waziri wa Utalii
na Mambo ya Kale, Mudrik Ramadha Soraga
na watendaji wa wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment