Habari za Punde

Matukio ya Picha Kutoka Banda la Maonesho la Tanzania katika Mkutano wa COP29

Wageni mbalimbali wakitembelea na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za hifadhi ya mazingira katika banda la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.

Wageni mbalimbali wakitembelea na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za hifadhi ya mazingira katika banda la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.

Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Kenya Abdi Dubat (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa na Mhandisi Mwanasha Tumbo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, walipotembelea banda la Tanzania katika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendelea jijini Baku nchini Azarbaijan.

Wajumbe kutoka Tanzania, Msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Emma Liwenga pamoja na Afisa Kiungo wa Masuala ya Kaboni Dkt. Deo Shirima akifanya mazungumzo na Mwekezaji kutoka Brazili Bw. Lap Tak Chan ambaye ameonesha nia ya kuwekeza katika biashara ya kaboni kwenye misitu ya asili iliyopo nchini Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Ignas Chuwa kwenye banda la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.