Habari za Punde

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Namibia Mhe. Anne Makinda Akutana na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Namibia

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- SEOM), nchini Namibia Mhe. Anne Makinda tarehe 19 Novemba 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Namibia Bi. Rebecca Liyambo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Bi. Rebecca Liyambo ameikaribisha SEOM nchini Namibia na kumshukuru  Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Namibia wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- SEOM), Mhe. Anne Makinda na ujumbe wake kwa kumtembelea ofisini

Ameiahidi SEOM Ushirikiano ili kuiwezesha kutekeleza jukumu lake la Uangalizi kwa tija na ufanisi .

Amesema jukumu la uangalizi wa uchaguzi linalenga kuhakikisha uwepo wa uwazi na uaminifu wa mchakato wa uchaguzi, na kuongeza kuwa kazi hiyo ni muhimu katika kuimarisha imani ya umma kwenye uchaguzi na kuchangia ustawi na maendeleo ya nchi wanachama wa SADC.

Katika tukio lingine Mhe. Makinda amekutana na kuzungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za SADC nchini Namibia ambao wameelezea kuridhishwa kwao na hali ya ulinzi na usalama nchini humo kipindi hiki wakielekea katika uchaguzi mkuu.

Mabalozi hao wameipongeza Serikali na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Namibia  kwa jitihada kubwa za kuimarisha ulinzi, usalama na amani kwa wananchi wake kwani hali hiyo itawawezesha wananchi wa Namibia kutekeleza haki yao ya msingi na ya kidemokrasia ya kupiga kura kwa amani na utulivu.

Wakati huo huo Mhe. Makinda amekutana na kuzungumza na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Namibia Meja Jenerali Anne-Marie Nainda, aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo.

Meja Generali Anne-Marie Nainda,  amesema askari 5,042 wa kulinda la amani wanatarijiwa kusambazwa katika mikoa yote ya nchi hiyo hali ambayo alielezea kuwa itasaidia kudhibiti machafuko ya kisiasa endapo yatatokea wakati wa kampeni za uchaguzi na wakati wa uchaguzi baada ya matokeo ya Washindi hutangazwa rasmi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.