Habari za Punde

Serikali ya Awamu ya Nane(8) ni kuwatumikia Wazanzibari hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amba pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na kulifungua Kongamano la Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekjiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa ( UWT)  lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifua Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema kazi ya Serikali ya Awamu ya Nane(8) ni kuwatumikia Wazanzibari hasa katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Ameyasema hayo katika ufunguzi wa Kongamano la Kumpongeza Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa ( UWT)  lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.

Amesema Serikali itaendela kuwafikia na kuwawezesha wajasiriamali wote nchini   ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na kukuza mitaji ya biashara zao kwa faida yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Hemed amesema miradi mbali mbali inayoendelea kujengwa na Serikali kwa Unguja na Pemba ambayo imemgusa kila mwanachi wa Zanzibar hivyo ipo haja na hoja ya kuendelea kuyatangaza mazuri yanayofanywa na viongozi wakuu wa nchi.

Sambamba na hayo Mjumbe huyo wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa amewataka UWT kufanya kazi kwa pamoja ya kukitafutia kura za ushindi Chama cha Mapinduzi kwa kuwashajihisha wananchi  kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili waweze kupata fursa ya kuipigia kura CCM na kuendelea kushikilia dola ifikapo mwaka  2025.

Nea Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. ZAINAB KHAMIS SHOMARI amesema Utekelezaji wa Ilani katika kipengele cha kuwawezesha wanawake kimetekelezwa kwa kiasi kikubwa ambapo wanawake wamekuwa wakinufaika kupitia program mbali mbali zinazotekelezwa na Serikali za kuwawezesha wananchi kiuchumi.

SHOMARI amesema UWT imejipanga kuwafikia na kuwawezesha wanawake wengi wa Zanzibar kwa kuwapatia mikopo yenyenye Thamani ya Shilingi Milioni 75 zitakazotolewa kwa wanawake wa Mkoa wa kaskazini Pemba ambapo Milioni 170 zitatolewa kwa Pemba nzima

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT Taifa Ndugu SUZAN PETER KUNAMBI amesema Serikali ya Awamu ya Nane imefanya mambo mengi ambayo yanawanufaisha wanawake katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii ndani ya Zanzibar.

Suzan amesema wanawake wa  UWT watahakikisha  kuwa namna yoyote ile Rais Dkt Mwinyi anapata kura  nyingi za heshima zitakazomuwezesha kuendelea kuiongoza Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wake  kwa miaka mitamo ijayo.

Ameiomba Serikali kuendelea kuwatumia wataalamu wanawake katika harakati mbali mbali za Chama na Serikalini ikiwemo kuwapa nafasi na kuwaamini katika kusimamia miradi ya maendele inayoendelea kujengwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Imetolewaa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 31. 10 . 2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.