Habari za Punde

Amewahimiza Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuendelea Kuiombea Nchi Amani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizngumza na kumulia hali Muazilishi wa Madrasatul Maryam Mfenesini Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja,Bi.Maryam Omar Muhammed, kabla ya kuaza kwa Dua maalumu ya kumuombea , iliyofanyika leo 29-12-2024.  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Viongozi na  Waumini wa dini ya Kiislamu  kuendelea kuiombea nchi amani  wakati huu  ikielekea  kipindi cha Uchaguzi Mkuu  wa mwaka 2025.

Rais Alhaj Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipotoa salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu  wa Madrassa Maryam ya  Mfenesini Wilaya ya Kaskazini  B alipojumuika  katika Dua Maalum ya Kumuombea  ilioandaliwa na Madrassa.

Ameeleza kuwa  mambo yote ya Maendeleo yataweza kufanyika  ikiwa nchi itabaki na Amani  na Wananchi kuwa na Umoja  na Utulivu  wa nchi.

Amefahamisha kuwa hakuna nchi  yenye machafuko iliyopata Maendeleo hivyo kila mmoja ana wajibu wa  kusisitiza Amani  kwa maslahi ya nchi.

Alhaj Dk.Mwinyi  ameeleza kuwa Uzoefu unaonesha kuwa  kwa muda mrefu  nchi ilikuwa ikipata matatizo hususan wakati wa Uchaguzi  hivyo ni vema mambo hayo yasijirudie  tena kwa kuhubiri Amani  ndani ya Jamii.

Kabla ya Dua hiyo maalum Alhaj Dk. Mwinyi alimjulia  hali Mwanzilishi wa Madrassa hiyo    Bi.Maryam Omar Muhammed.











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.