Na.OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuchukua hatua mbali mbali kuimarisha huduma za afya sambamba na ujenzi wa miundombinu kwa ujenzi wa wa majengo zikiwemo nyumba za wafanyakazi.
Mhe. Othman ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa ACT- Wazalendo, ameyasema hayo hospitali ya wilaya ya Wete iliyopo Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Pemba alipozungunza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa hopsitali hiyo ikiwa ni shamra shamra za sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 61 .
Mhe. Makamu amesema kwamba hatua hiyo ya serikali pia inakwenda sambamba na uwekaji wa vifaa vya kisasa vya uduma za afya ili kuwapatia wananchi wa Zanzibar huduma bora za afya na kuhakikisa upatikanaji wa huduma za matibabu ya dharura ili kupunguza mazara kwa wananchi na vifo visivyotarajiwa.Amefahamisha kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafarajika kuona kwamba inaendelea kusimamia na kuhakikisha watoa huduma za afya wanapatiwa makaazi bora ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi na kuoneza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Mhe. Makamu amesema kwamba ujenzi wa Makaazi karibu na hospitali ama vituo vya afya kutasaidia kuwapunuzia masafa na gharama za usafiri wa kuwafata madaktari bingwa na wafanyakazi wengine jambo linaloimarisha huduma za matibabu ili wananchi wote wapate matibabu kwa wakati.
Hivyo, Mhe. Othman ametoa wito kwa uonozi wa wizara ya afya kuanza kufikiria namna bora na utaratibu sahihi wa kuzitunza nyumba hizo kwa kuzinatia kuwepo mpano wa kuzikarabati kwa wakati hasa kwa kuzingatia kwamba serikali inatumia gharama kubwa katika ujenzi wa nyumba hizo.
Kwa upande mwengine Mhe. Makamu amewaomba wananchi hasa wawilaya hiyo na maeneo jirani kuendelea kutoa mashirikiano kwa kuitumia hospitali hiyo ipasavyo kwa kufanya uchunguzi wa maradhi kwa kufuata utaratibu wa rufaa wa matibabu kwa mujibu wa miongozo ya wizara ya afya inavyoelekeza.
Mhe. Othman ameeleza haja ya wananchi kujitahidi kujikinga na maradhi mbali mbali kwa kuwa kinga ni bora kulikotiba na kwamba kufanya hivyo kutaipunguzia serikali mzigo wa gharama za kuwatibu wananchi wanaopata ugonjwa ambao uneweza kutibika.
Kwa upande mwengine Mhe. Othman ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kushirikiana na wizara ya Afya kuhakikisha kipande cha barabara inayoingia hospitali hiyo kutoka eneo la barabara kuu ya Kinyasini hadi hospitali hapo inajengwa ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa hasa mama wa wajawazito kuepuka kujifungua njia.
Nyumba hizo zinazojenwa zinatarajiwa kuchukua jumla ya familia kumi na sita na zinatarajiwa kuwa ni msaada mkubwa kwa madaktari na wafanyakazi wengine katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Akimkaribisha Mhe, Makamu , waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazurui amesema kwamba dhamira ya wizara hiyo ni kuhakikisa upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi na pia kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kutenmgeneza mazingira mazuri ya utoaji huduma kwa umma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema kwamba ujenzi wa nyumba hizo ni sehemu ya kuendeleza miradi ya maendeleo kutimiza lengo la mapinduzi na kwamba mwaka huu jumla ya miradi 16 itawekewa mawe ya msingi , kuzinduliwa na mingine kufunguliwa mwaka huuu ndani ya mkoa huo.
Akitoa taarifa ya Kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Miraji Mzee Mgereza amesema kwamba mradi huo hadi utakapokamilika utagharamu serikali ya mapinduzi ya Zanzibar jumla ya shilingi bilioni 4.1 na utaondoa usumbufu kwa madaktari na wafanyakazi wengine katika hospitali hiyo.
Kilele cha sherehe za kutimia miaka 61 tangu Mapinduzi ya Januari 1964 zinatarajiwa kufanyika Kisiwani Pemba Januari 12 mwaka 2025 na hivi sasa serikali ipo kwenye uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa miradi mbali mbali ya maende leo.
MWISHO
Imetolewa na ofisi ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha habari leo Jumanne Disemba 24.2024.
No comments:
Post a Comment