Habari za Punde

ELIMU YA FEDHA YAFIKA MKOANI ARUSHA

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akizunguza katika Ofisi ya Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Jonas Mwita (hayupo pichani), baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha katika mkoa huo.  
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro (wakwanza kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita, Nyenzo ya Kufundishia Elimu ya Fedha baada ya Timu hiyo ya kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufika katika Ofisi yake jijini Arusha.
Afisa Mwandamizi, Uchambuzi Fedha, Idara ya Sera, Utafiti na Mipango, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA. Gladness Mollel, akitoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Jiji la Arusha, kuhusu masuala ya uwekezaji.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoani Arusha, Bw. Josephat Komba, akieleza faida za wajasiriamali kujiunga na Mfuko huo,  baada ya wajasiriamali hao kujitokeza katika Ukumbi wa  Arusha Sekondari kwa ajili ya kupata elimu ya Fedha kutoka kwa Wataalam kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali.

Afisa Matekelezo uchangiaji hiari Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Arusha, Bi. Marietha Ngoma, akitoa elimu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuhusu uwekezaji kupitia mfuko huo, walipoungana na Timu ya Wataalam wa kutoa Elimu ya  fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi na wadau wengine jijini Arusha.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akitoa ufafanuzi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha, kuhusu filamu ya elimu ya fedha yenye ujumbe kuhusu masuala ya uwekezaji, utunzaji wa fedha binafsi, kuweka akiba, kusajili vikundi vidogo vya fedha pamoja na masuala ya mikopo ambapo Timu ya wataalamu wa elimu wa fedha inatarajiwa kutoa elimu hiyo katika Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.