Akitoa shukurani katika Iftari hiyo Alhajj Hemed amewashukuru Viongozi na Wananchi waliofika katika Iftari hiyo na kueleza kuwa mkusanyiko huo unaleta umoja katika jamii.
Aidha amewakumbusha waumini wa dini ya kiislamu
kuendeleza tabia ya kuhurumiana na kusaidiana kwa kutoa
walivyonavyo kwa makundi maalum ikiwemo Mayatima,
Wazee, Wajane na Watu wenye Ulemavu hasa katika kipindi
hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Amewasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani na
utulivu kabla, wakati na baada ya uchaguzi ili kutoa fursa kwa
serikali kuijenga zanzibar kimaendeleo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idriss Kitwana
Mustafa amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwa kuendeleza Ibada hiyo ya kufuturisha ikiwa ni kawaida kwa
Viongozi na Waumini kufuturishana ndani ya Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment