Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa na Naibu Mawaziri mbalimbali, akishiriki
kikao cha Bunge cha uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka
wa fedha 2025/26 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba
bungeni jijini Dodoma tarehe 12 Juni 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian
Luhemeja (wa pili kulia) akiwa na viongozi mbalimbali, akifuatilia kikao cha
Bunge cha uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2025/26 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba bungeni
jijini Dodoma tarehe 12 Juni 2025.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba bungeni jijini
Dodoma leo tarehe 12 Juni 2025 akiwasilisha Hotuba ya Bajeti
Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 bungeni jijini
Dodoma tarehe 12 Juni 2025.
Serikali imesema Muungano ni
tunu adhimu ambayo imesaidia kuendelea kufikia malengo
ya nchi kwa
vipindi tofauti tangu kuasisiwa kwake hivyo imewataka Watanzania kuendeleza
upendo na mshikamano uliopo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameliarifu Bunge wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma leo tarehe 12 Juni 2025 ambapo amesema fedha za utekelezaji wa miradi zimepatikana.
Amesema katika kuhakikisha nchi inakuwa na
uhimilivu wa kiuchumi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, inatekeleza programu
mbalimbali za uhifadhi wa mazingira.
Mhe. Nchemba amesema kuwa pamoja na masuala mengine programu za uhifadhi wa mazingira zinahusisha maboresho ya sheria, kanuni na taratibu mbalimbali.
Alifafanua kuwa Serikali imeendelea kunufaika na programu mbalimbali za
uhifadhi wa
mazingira kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ikiwemo Shirika la Fedha la
Kimataifa (IMF) kupitia dirisha la Resilience
and Sustainability
Facility (RSF).
“Naomba niwahikikishie Serikali ya Awamu ya
Sita inaendelea kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi zikiwemo utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022 – 2032) ambao unalenga kutatua changamoto
za mazingira nchini,” alisema.
Dkt. Nchemba aliongeza kuwa Serikali imeanzisha Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) ili kuimarisha usimamizi na kunufaika zaidi na biashara ya kaboni nchini.
Hivyo, Waziri Nchemba ameliomba Bunge ridhaa ya kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 56.49 kwa mwaka wa fedha 2025/26.
No comments:
Post a Comment