Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Katika Sala ya Ijumaa na Sala ya Maiti Kumsalia Marehemu Abdallah Ali Mfaume Iliyofanyika Masikiti wa Ijumaa Miembeni Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume, kwa kufiwa na Kaka yake Abdallah Ali Mfaume, alipowasili katika viwanja Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya Sala ya Ijumaa na Sala ya Maiti iliyofanyika katika msikiti huo, baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa leo 13-6-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali,alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya Sala ya Ijumaa,iliyofanyika leo 13-6-2025 na Sala ya Maiti kumsalia marehemu Abdallah Ali Mfaume, Kaka wa Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika kubeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Abdallah Ali Mfaume, kwa ajili ya Sala ya Maiti iliyofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja, baada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 13-6-2025 katika msikiti huo na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Sala ya Maiti kumsalia marehemu Abdallah Ali Mfaume, iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 13-6-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Abdallah Ali Mfaume, ikisomwa na Sheikh.Sameer Zulfikar,baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, kumsalia marehemu Abdallah Ali Mfaume, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 13-6-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Abdallah Ali Mfaume, ikisomwa na Sheikh.Sameer Zulfikar,baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, kumsalia marehemu Abdallah Ali Mfaume, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 13-6-2025
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.