Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini
Dodoma leo tarehe 11 Juni 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito huo
wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Zaytun Swai aliyetaka kujua kuna mkakati gani kuvutia wawekezaji wa biashara ya kaboni katika Mkoa wa
Arusha.
Pamoja na wito huo,
amesema Serikali itaendelea kutafuta masoko ambapo tayari wawekezaji wamejitokeza
kuwekeza katika halmashauri za wilaya za Karatu na Monduli mkoani Arusha ambazo
niThe Nature Conservancy (TNC), Albrin (Sandrose), Soils for
the Future Tanzania (SftTZ) na Carbon.
Pia, Mhe. Khamis amesistiza Serikali itaendelea kusimamia sheria, kanuni
miongozo na taratibu, katika uendeshaji wa biashara hii ili wananchi wavutiwe na
wanufaike na uwepo wa biashara hiyo.
Akiendelea kujibu swali hilo, alisema
Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) kwa
kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI inatekeleza mikakati mbalimbali
kuvutia wawekezaji wa biashara hiyo katika Mkoa wa Arusha.
Mhe. Khamis alitaja mikakati hiyo kuwa ni mbali ya kuanzisha kisheria NCMC sanjari
na Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa Biashara ya Kaboni (2022), ambazo
zimefanyiwa marekebisho mwaka 2023.
Halikadhalika, Kutoa elimu kwa umma kuhusu biashara ya kaboni imeendelea
kutolewa pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika biashara hiyo
zikiwemo ambazo.
Kwa upande mwngine, Naibu Waziri Khamis alisema kutokana na uwepo wa misitu
mikubwa upande wa Zanzibar, visiwa hivyo vinakwenda kunufaika na matunda ya
biashara ya kaboni.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira
ya Zanzibar (ZEMA), wawikilishi, wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na mawziri
kutoa kutoa elimu kwa wananchi wa visiwa hivyo kutunza miti ili kunuifa na
biashara ya kaboni.
Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Amani Mhe. Abdul Yussuf
Maalim aliyetaka kujua kuna mkakati gani wa kuwashirikisha wadau wa Zanzibar
ili waweze kunufaika na biashara ya kaboni.
Hivyo, biashara ya kaboni imeendelea kuleta manufaa kwa Serikali na kwa
wananchi kwa ujumla hususan katika halmashauri zinazozunguka misitu hapa nchini
kwa kujengewa miundombinu kutokana na mapato yanayotokana na biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment