Na Oscar Assenga Tanga
FEDHA zilizotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 kwa ajili ya uwekezaji katika bandari ya Tanga, fedha hizo zimerudi na kubaki salio la shilingi bilioni 56.7.
Hayo yalisemwa na Meneja wa bandari ya Tanga Mhandisi Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa kwa kipindi cha miezi 24 taasisi mbili za serikali za TPA na Mamlaka ya mapato nchini TRA, wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 484.8.
Alisema kutokana na makusanyo hayo ile fedha iliyotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 imesharudishwa na taasisi mbili za TPA na TRA kwa miezi 24 na chenji pembeni imebaki na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huo.
Akifafanua kuhusu makusanyo hayo alisema kwamba TPA imeendelea kuvunja rekodi ya mapato kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali na kupelekea ongezeko la shilingi bilioni 30 ya mapato ambayo waliwekewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 45.56 hadi kufikia makusanyo ya shilingi bilioni 75.139.
Aidha alisema katika mwaka wa 2023/2024 Bandari ya Tanga iliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 38.7 tofauti na makusanyo ya shilingi bilioni 75.139 ikiwa ni ongezeko la asilimia 94.
Meneja huyo alisema makusanyo hayo ni kwa taasisi mbili za serikali ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka wa fedha 2024/2025 waliweza kukusanya shilingi bilioni 215 kati ya hizo Bilioni 107 zimetoka Bandari ya Tanga kupitia mizigo mchanganyiko.
Pia alisema kwa upande wa makusanyo ya mafuta waliweza kukusanyia kiasi cha shilingi bilioni 108 hivyo ukichukua makusanyo hayo kwa taasisi hizo ni kiasi cha shilingi bilioni 215.22 na TPA wamekusanya shilingi bilioni 75.159 na kufanya jumla kuwa shilingi bilioni 290 ambazo zimeweza kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kipindi cha miezi 24.
Aliongeza kutoka mwaka 2023/2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA) waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 195 na ni taasisi mbili tu kwa mchanganuo huo kwamba TPA walikusanya Bilioni 38.7 na TRA walikusanya Bilioni 156.75 hiyo jumla yake ni zaidi Bilioni 195.
Alieleza kwamba ukichukua miezi 24 mwaka 2023/2024 ilikuwa ni Bilioni 195 na pointi zake na 2024/2025 nilikuwa ni bilioni 290 ukizijumulisha zote unapata kwa miezi 24 TRA na Bandari ya Tanga imeweza kukusanya Bilioni 485.8.
Meneja huyo alisema kwamba katika Bandari ya Tanga June 30 mwaka huu, mwaka wa fedha uliomalizika wameweza kuhudumia shehena tani milioni 1,416,127 wao wamefanikiwa kuhudumia mertiki tani milioni 1,326,415.
Alieleza katika mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 bandari iliweza kuhudumia metric tani milioni 1,191,480 ukichukua tofauti ya mwaka huu na mwaka 2023/2024 na mwaka 2024/2025 waliohudumia watapata tofauti ya laki 1,340,000 utaona kuna ongezeko la asilimia 11.3 kati ya mwaka 2023/2024 na mwaka 2024/2025 bandari imeweza kuongeza kiwango cha kuhudumia shehena.
Akizungumzia kuhusu meli zilizohudumiwa na Bandari hiyo alisema kwamba walipewa lengo la kuhudumia meli 222 lakini kwa mwaka wa fedha 2024/2025 baada ya kupewa malengo hayo wameweza kuhudumia meli 458 katika meli hizo meli 148 za Bahari kuu na Meli 310 ni za Mwambao.
Mwaka 2023/2024 Bandari ya Tanga iliweza kuhudumia meli 307 utaona kuna tofauti ya meli 151 ni sawa na asilimia 49.1 wameongeza idadi ya kuhudumia meli zaidi na upande wa makasha walipewa lengo la kuhudumia makasha 8,351 lakini wamefanikiwa kwa mwaka wa fedha 9,026 ni ongezeko la asilimia 8 lakikni mwaka 2023/2024 waliweza kuhudumia makasha tools 7,817 ukiangalia ni ongezeko la asilimia 15.46 ,
Upande wa abiria mwaka 2024/2025 walipewa lengo la kuhudumia abiria 120,000 lakini hawakufanya vizuri waliweza kuhudumia kwa asilimia 50 ambapo abiria 59,960 waliweza kuhudumiwa kwa kipindi cha mwaka 2024/2025.
Alisema mwaka wa nyuma yake 2023/2024 waliweza kuhudumia abiria 62,904 hiyo kwa sababu katika eneo hilo ni wadau binafsi wenye meli ndio wenye jukumu la wa kuwasafirisha abiria kutoka Tanga kwenda maeneo mengine kama Zanzibar maeneo ya Pemba na Unguja
Mwisho.
No comments:
Post a Comment