Habari za Punde

WANANCHI WATAKIWA KUFAHAMU MNYORORO WA UGAVI

Afisa Ugavi Mwandamizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi (wa pili kulia) akipewa mkono wa pongezi na Msanii wa Sanaa ya Uchekeshaji, Bw. Mtanga Hamis, maarufu Mtanga,baada ya kupata elimu ya ugavi, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu, kulia ni Afisa Ugavi, wa Idara hiyo, Bi.Anne Swila na wa pili kushoto ni Msanii wa Sanaa ya Vichekesho, Bw. Dickson Malwaya, maarufu kama Bambo.

Na. Peter Haule na Chedaiwe Msuya, WF, Dar es Salaam

Wananchi wametakiwa kufahamu mnyororo wa ugavi ambao ni sehemu muhimu yenye mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya Serikali hasa katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
 
Hayo yamesemwa na Afisa Ugavi Mwandamizi kutoka Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi (wa pili kulia) alipokuwa akitoa elimu kuhusu mnyororo wa ugavi kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
 
Alisema kuwa mnyororo wa ugavi ni mtangamano wa shughuli za ununuzi, ugomboaji, upokeaji, urejeshaji, utunzaji, uhifadhi na matumizi, usambazaji na uondoaji wa bidhaa, vifaa au mali za umma.
 
Bi. Vaileth alisema kuwa,  mtangamano huo unalenga kutimiza matarajio ya wananchi ya kupata huduma toshelevu na thamani halisi ya fedha zinazotumika katika shughuli za mnyororo huo.

Kwa upande wa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha walisema kuwa maelezo ya wataalamu na machapisho ya kielimu walioyapata bandani humo yamewasaidia kuelewa kwa undani masuala ya mnyororo wa ugavi.

Banda la Wizara ya Fedha linahusisha wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Wizara hiyo na Taasisi zake ikiwa ni pamoja na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Mary Mihigo akitoa elimu kwa kazi wa Dar es Salaam, Bw. Sarah Njau, kuhusu akiba, mikopo na uwekezaji alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha  Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally, akijibu maswali kuhusu pensheni inayotolewa na Hazina kwa wananchi walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindimo akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu kuhusu maandalizi ya bajeti ya Serikali.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, akitoa elimu ya deni la Serikali na deni la Taifa, kwa mkazi wa Temeke Dar es Salaam, Bw. Bausi Matumbo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
      (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.