Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akimuwakilisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika dua ya kuiombea nchi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu Pemba na kufanyika katika Masjid RAHMAAN Gombani Pemba.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwahimiza vijana wao katika kuitunza amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika dua ya kuiombea nchi iliyoandaliwa na ofisi ya mufti mkuu kanda ya Pemba na kufanyika katika Masjid Rahman uliopo Gombani Pemba.
Amesema kuwa ni lazima kukaa pamoja na kushirikiana kwa kila jambo ili kuhakikisha wanapiga vita viashiria vyote vya uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa bila ya amani hakuna chochote cha kimaendeleo kinachoweza kufanyika nchini.
Alhajj Hemed amefahamisha kuwa wazizi na walezi ndio wahusika wakuu katika kuwaandalia vijana mazingira wezeshi ili kuweza kuishi katika hali ya amani na utulivu sambamba na kuyafaidi matunda ya kimaendeleo yanayoendea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya Nane.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka waumini kutokukubali kushawishiwa kuingia katika uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha siasa jambo ambalo sio sahihi.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewashukuru waumini kwa kuendelea kuiombea dua nchi hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Kwa upande wake Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. MAHMOUD MUSSA WADI amewataka waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa ujumla kuiombea dua nchi na viongozi wake kila wakati ili Mwenyezi Mungu aweze kuiepusha nchi na machafuko hasa kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi.
Sheikh Mahmoud amesema historia inaonesha kuwa nchi nyingi duniani kila ifikapo kipindi cha uchaguzu hupatwa na taharuki ya kutoweka k wa amani katika nchi zao hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anailinda amini kwa gharama yoyote kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe..25.09.2025.
No comments:
Post a Comment