Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla alipowasili Kwenye viwanja vya Kwareni kuzindua wa kampeni za uchaguzi za CCM Jimbo la Kiwani Pemba, Septemba 21, 2025.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa Mohammed Abood (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Rashid Hadidi Rashid (wa pili kushoto) na Mwenyekiiti wa CCM Mkoa wa Kusini, Yufuf Ali Juma, alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba ambako alizindua kampeni uchaguzi za CCM Jimbo la Kiwani Zanzibar, Septemba 21, 2025.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua kampeni za uchaguzi za CCM katika Jimbo la Kiwani kwenye Uwanja wa Kwareni , Pemba , Septemba 21, 2025.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimejipanga kuendelea kuleta maendeleo katika sekta zote nchini.
Amesema kuwa Chama hicho mara zote kimekuwa kikigusa maendeleo kwa watanzania katika sekta zote hivyo kukichagua katika uchaguzi wa mwezi Oktoba 2025 ni uamuzi wa kuchagua maendeleo.
Amesema hayo leo Jumapili (Septemba 21, 2025) alipozindua kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Kiwani, katika viwanja vya Kwareni, Pemba Zanzibar. Mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.
"Wote ni mashahidi, Pemba ya leo, Zanzibar ya leo ni tofauti na tulipotoka, hatua za kimaendeleo katika maeneo haya ni mkubwa na yanaonekana kila sekta imeguswa, Mimi pia ni shahidi, nilifungua kituo cha afya hapa na sasa ninaambiwa kinatumika na mnanufaika nacho".
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa Wazanzibar kuchagua wagombea Urais wa CCM kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar kwa kuwa wameonesha wanaweza kusimamia maendeleo katika maeneo yao.
"Rais Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi ni madaktari wa maendeleo, hawa wote ni wasikivu waadilifu waaminifu na wapenda maendeleo wachagueni viongozi hawa ili wafanya kazi nanyi, hawa ni wapenda maendeleo namba moja, wanasikiliza kero na kuzifanyia kazi"
Kwa upande wake mgombea Uwakilishi wa Jimbo hilo, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewaahidi wananchi wa Jimbo hilo kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa na ndani ya miaka mitano atazitatua changamoto katika eneo hilo.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake, atahakikisha kila kijana anayetoka katika jimbo hilo na kwenda kusoma popote watamfuatilia ili kusimamia maendeleo yake na kumuwezesha kunufaika na jitihada zake.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimnadi mgombea wa kiti cha Uwakilishi katika Jimbo la Kiwani, Pemba ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla wakati alipozindua kampeni za uchaguzi za CCM katika Uwanja wa Kwareni , Pemba, Septemba 21, 2025.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025/2030 mgombea wa kiti cha Uwakilishi katika Jimbo la Kiwani, Pemba ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla wakati alipozindua kampeni za uchaguzi za CCM katika za Jimbo hilo kwenye Uwanja wa Kwareni , Septemba 21, 2025.
Wanananchi wa Pemba walioshiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM Jimbo la Kiwani Pemba kwenye uwanja wa Kwareni, Septemba 21, 2025. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mjumbe wa kamti Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment