Habari za Punde

KARUME BOYS YATOKA SARE NA RWANDA CECAFA 1-1

USHINDI DHIDI YA YEMEN MASHAKANI
Timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zanzibar - Karume Boys imetoka sare na timu ya vijana ya Rwanda katika mashindano ya Cecafa yanayoendelea Asmara - Eritrea jana.

Beki wa Karume Boys, Saleh Ahmed alijifunga mwenyewe katika dakika ya 35 wakati akipapatua kuokoa krosi ya wanyarwanda ambao walichezesha kikosi chao cha chini ya umri wa miaka 17 kinachojiandaa na mashindano ya Afrika.


Karume Boys walifanikiwa kupata penelti katika dakika ya 74 ambayo ilipigwa na Ventrous Kamanya kusawazisha katika mchezo ambao muda mwingi ulichezwa huku kukinyesha mvua mkubwa.

Katika mchezo hu ambao ulikuwa wa kibabe, mchezaji mmoja wa Zanzibar alitolewa kwa kadi nyekundu wakati wachezaji wawili wa Rwanda pia walitolewa na Refa David Sagaro kutoka Kenya.

Hata hivyo ushindi wa Zanzibar dhidi ya Yemen umeingia mashakani baada ya kuchezesha mchezaji mmoja anaedhaniwa kuwa na umri mkubwa kwani kwenye hati yake ya kusafiria imeonesha amezaliwa 1989 wakati wachezaji wanaokubalika ni kuanzia waliozaliwa 1991.


Endapo ushindi huo utabatilishwa, ili kuweza kusonga mbele, Karume Boys itabidi iwafunge Uganda kesho katika mchezo wa mwisho. Uganda tayari wameshafuzu nusu fainali baada ya kuwafunga Wayemen 3-2.

ZANZIBAR - 19. Gharib Musa: 7. Salum Said, 6. Idrissa Abdulrahim (captain), 20. Juma Othman, 14. Ali Juma Hassan, 16. Mbaruk Ali (18. Mohamed Juma, 46’), 5. Ahmed Saleh, 3. Makame Hamad (11. Mohamoud Ali, 46’), 9. Ali Othman, 10. Ventrous Kamanya, 17. Ali Badru
Wachezaji wa akiba - 1. Rashid Haji, 2. Maulidi Ramadhan, 8. Ishak Othman, 12. Renatus Morris, 13. Ibrahim Rajab, 15. Suleiman Ali

Wafungaji - 5. Ahmed Saleh, (amejifunga mwenyewe, 35’), 10. Ventrous Kamanya - Penelti (74’)
Coach - Abdel Al Fatah (Misri)

RWANDA - 1. Marcel Nzarora: 2. Michel Rusheshangoga, 15. Faustin Usengimana, 8. Emery Bayisenge, 5. Eric Rutanga (3. Celestin Ndayishimiye, 75’), 6. Robert Ndatimana, 16. Patrick Umwungeri, 17. Jean-Paul Rulisa, 9. Isaie Songa (10. Innocent Mugabo, 74’), 12. Justin Mico, 11. Innocent Habyalimana

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.