Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban akifatilia Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
Na Chedaiwe Msuya, WF, Washington D.C, Marekani
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameshiriki katika Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichojadili fursa na changamoto za matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika usimamizi wa uchumi jumla kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington DC, Marekani.
MEFMI ni taasisi ya kikanda inayolenga kujenga uwezo wa nchi wanachama katika usimamizi wa sera za uchumi jumla, masuala ya fedha, usimamizi wa madeni, pamoja na takwimu za kiuchumi.
Majadiliano ya kikao hicho yalijikita katika kuchunguza namna AI inaweza kuchangia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, uchakataji wa data kwa ajili ya maamuzi ya kisera na uwekezaji, upangaji na ugawaji wa rasilimali fedha, pamoja na utoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, kikao hicho kilibainisha changamoto zinazokabili utekelezaji wa teknolojia ya AI katika nchi zinazoendelea, ikiwemo uhaba wa miundombinu thabiti, ukosefu wa takwimu sahihi, upungufu wa wataalam wenye umahiri wa kiteknolojia, na masuala yanayohusu usalama na usiri wa taarifa.
Kwa pamoja, nchi wanachama zilikumbushwa umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, kujenga uwezo wa kitaasisi na kitaalam, pamoja na kuandaa sera na miongozo itakayohakikisha matumizi salama, yenye maadili na uendelevu wa teknolojia ya AI.
Matumizi sahihi ya AI yana uwezo mkubwa wa kuimarisha usimamizi wa uchumi, kuongeza ufanisi wa taasisi, na kuiwezesha Afrika kusonga mbele katika kukuza uchumi shindani na jumuishi kwa manufaa ya wananchi wake.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila akifatilia Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Fedha wakifuatilia Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban akiteta jambo na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), kilichofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Fedha wakifuatilia Kikao cha Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Jumla na Fedha kwa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), inayoendelea jijini Washington D.C, Marekani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Washington D.C, Marekani)
No comments:
Post a Comment