Habari za Punde

TUSAIDIANE KATIKA KUCHANGIA MAWAZO YA KUWAJIBU WADAU

Natumai hujambo pamoja na ndugu na jamaa wototo huko uliko mimi namshukuru allah alhamdulilah.
Zaidi ni kwa masikitiko makubwa nimeamua kukutumia ujumbe huu kwani nilikua kwenye mtandao kufuatilia khabari za nyumbani na yanayojiri lakini naona bado upo nyuma sana kwa kutujulisha yanayopita kwenye blog yako na la kutilisha unyonge zaidi ni kwamba nimeranda kwenye kila pembe za mitandao kulitafuta gazeti letu la kizanzibari halimo kwenye ramani ya dunia naona ni kweli yasemwayo sisi mwisho wetu ni chumbe tu kwa maana magazeti yooote ya tanganyika unayapata kwenye google ila zanzibar leo halipatikani popote zaidi ya mrima nimeliona likichambuliwa kwenye chanel 10 nikapata hamu ya kusoma lakini wapiiiiiiiiiiii haiwezekani au vipi kaka yangu mmefunwa midomo mikono elimu zenu pia zimetawaliwa uhuru wenu uko wapi? haki zenu juu ya kazi zenu ziko wapi? na usawa wa hao ndugu zetu upo wapi? na kwanini wao waweze sisi tusiweze bado mmekaa kimya mnaogopa kitumbua kisiingie mchanga mnasahau kama rizki anaetoa ni allah hii dunia ni mapito tuu na mtaulizwa kwa muumba jee uliisimamia vipi haki kwa kumukhofu mja ukasahau aliekuumba kwa kweli inauma tena inauma sanaaaaaaaaaaaaa ila kila lenye mwanzo lina na mwisho .
Natanguliza kuomba msamaha kama haya utayaona yamekuchoma ila mimi nimesimama na nguzo ya allah huo ndio ukweli na lazima tuambizane tumkhofu m/mungu zaidi kuliko mwanadam nisameh kaka yangu si mimi ila nafsi imenituma na kuombana radhi ndivyo alivyotuagiza allah s.w..mimi ni yule yule mdau wako
NA HUYU MWENGINE


Kwanza nakupa shukurani sana kwa kuweza kufika kiwango cha kuweza kuwa mpiga picha wa kiwango cha kutumainiwa. Kaka yangu Othman nakuomba ujitahidi kuweza kutuwekea habari za picha kwa haraka zaidi. blog yako ni nzuri tunajaribu kuangalia kila siku hapa uk, najuwa lazima habari ziwe na chazo kinachoaminika lakini hizo za picha jitahidi.


Mara nyingi tuona habari zako huwa zishapitwa zinakuwa hazina ubora sana, kwa hivyo watu huwa hawafungui kwa kujuwa hawatopata habari motomoto, hukimbilia kufungua blog nyengine.

Natumai utaongeza juhudi za kupatika na habari zaidi na sisi tuweze kutegemea blog yako kama ndio kipasha habari za nyumbani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.