Habari za Punde

DK SHEIN AMTEUA JAJI OMAR OTHMAN MAKUNGU KUWA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu ambae ameteuliwa rasmi na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. Jaji Makungu anachukua nafasi iliyokuwa katika utumishi wa Mheshimiwa Iddi Pandu Hassan kwa kipindi kirefu ambaye amekuwa akiugua kwa muda mrefu.

Jaji Makungu kabla ya kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu amewahi kushika nafasi kadhaa za uongozi tokea alipoingia katika utumishi wa Serikali kama Mwanasheria wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na baadae kuwa Katibu Mkuu. Pia aliwahi kuwa Kamishna katika Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar na Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Jaji Makungu ana shahada ya uzamili katika taaluma ya Sheria.
 
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Othman Makungu akila kiapo cha utifu mbele ya Rais wa Zanzibar huku akishuhudiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk Abdulhamid Yahya Mzee hapo ikulu jana
   
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akimkabidhi hati yake ya kiapo pamoja na majukumu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Jaji Omar Makungu     
Pichani kutoka kushoto ni Jaji Mkuu Hamid Mahmoud, Mwanasheria Mkuu Jaji Omar Makungu, Rais wa Zanzibar Dk Shein, Spika aliyemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Dk Abdulhamid Yahya Mzee
RAIS wa Zanzibar Dk  Ali Mohammed Shein akipiga picha ya pamoja na Jaji Omar Othman Makungu

Wengine waliohudhuria katika hafla  hii ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mstahiki Meya wa mji wa Zanzibar Mhe. Mahboub Juma Issa, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Katiba na Utawala Bora Abdulghani Msoma pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Picha na Ramadhan Othman/ Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.