Na Rajab Mkasaba
SALAM za pongezi kutoka ndani na nje ya Tanzania zinaendelea kutolewa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, awamu ya saba.
Salamu hizo za pongezi zinatoka kwa Jumuiya, Vyama vya siasa, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mashirika, Wizara, Taasisi za serikali na zisizo za serikali, Afisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo nje na ndani ya nchi pamoja na wananchi mbali mbali.
Miongoni mwa salamu hizo ni kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania , Afisi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Devis Mwamunyange ambaye ametoa salamu za pongezi kwa Dk. Ali Mohammed Shein kwa niaba ya maafisa, askari, watumishi wa umma wanaofanya kazi Jeshini na kwa niaba yake binafsi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Salamu hizo zilieleza kuwa ushindi wa Dk. Shein umeonesha dhahiri imani kubwa waliyonayo wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla juu ya uadilifu alionao, uzalendo, uvumilivu, unyenyekevu na kwamba yeye ndiye atakayewaletea maendeleo ya kweli Wazanzibari wote chini ya mfumo mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Nao Ubalozi wa Tanzania nchini Kigali umeleta salamu za pongezi kwa Dk. Shein kwa kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano.
Salamu kutoka Ubalozi huo wa Tanzania nchini Rwanda zilieleza kuwa na imani kuwa Dk. Shein ataendelea kutumia hekima, karama na vipaji alivyonavyo sio tu katika kudumisha amani miongoni mwa Wazanzibari bali pia, kuendeleza mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo sasa chini ya maridhiano yaliyofikiwa hapo awali.
Sambamba na kuimarisha hali za maisha ya Wazanzibari walio wengi kwa kutekeleza kadri atakavyoweza ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Nayo Jumuiya ya Al-Youseif imetoa salamu za pongezi kwa Dk. Shein na kueleza kuwa watu wa Zanzibar wamefanya uchaguzi mzuri wa kumchagua Dk. Shein kutokana na uongozi wake bora.
Jumuiya hiyo, imemuhakikishia Dk. Shein kuwa itaendelea kutoa mashirikiano yake na misaada yake kwa Zanzibar.
Nae Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai CP Robert Manumba kwa niaba yake na watendaji wa Idara yake wametoa salamu za pongezi kwa Dk. Shein na kueleza kuwa kuchaguliwa kwake sio kwa bahati bali ni kutokana na juhudi zake katika kuchapa kazi.
Balozi Clement Geogre Kahama ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Udhamini Taifa la Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametoa salamu za pongezi kwa Dk. Shein kwa niaba yake na familia yake na kueleza kuwa ushindi wa Sk. Shein wa kubeba dhamana ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
No comments:
Post a Comment